Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Zerrin Sari

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Zerrin Sari is ni kiongozi muhimu wa Chama cha Mapinduzi na Ukombozi wa Watu/Front (Kwa Kituruki: Devrimci Halk Kurtuluş Partisi Cephesi, au DHKP/C). DHKP/C ililenga maslahi ya Marekani, ikijumuisha majeshi ya Marekani na wafanyakazi wa kibalozi pamoja majengo ya kibalozi tangu kuundwa kwake mnamo mwaka 1994 pale kundi tangulizi lake, Devinmci Sol au Dev Sol, lilipogawanyika. Lengo lake ni kutokomeza nyayo za Marekano na NATO toka Uturuki, na kujenga taifa la kijamaa. Mnamo Februari 2013, mtoaji mhanga wa bomu aliyehusishwa na kikundi hiki alishambulia ubalozi wa Marekani huko Ankara, kuua mlinzi wa kituruki. Serikali ya Mambo ya Nje iliitanza DHKP/C kuwa ni kundi la nje ya kigaidi tangu mwaka 1997, na kupitiwa upya na kufikiwa kwa hitimisho hilohilo tena mnamo Julai 24, 2013.

Zerrin Sari ni mwanasheria aliyefanya kazi ya kuitetea Dev Sol katika miaka ya 1990 mpaka pale alipokimbia Uturuki mnamo mwaka 1993. Alikuwa ameolewa to kiongozi muasisi wa DHKP/C Dursun Karatas, kwa pamoja walishirikiana kuandaa shughuli za DHKP/C huko Ulaya. Sari aishitakiwa na mahakama huko Ubelgiji mnamo mwaka 1999; na alitumia muda gerezani, na aliachiwa huru mnamo mwaka 2008, mwaka ambao Karatas alifariki kwa kansa. Inasemekana kisirisiri ni kiongozi wa DHKP/C, na inasadikika kuwa alitoa amri ya mashambulizi kwenye makao makuu ya Polisi ya Uturiki na makazi ya nyumba za polisi huko Ankara mnamo Septemba 20, 2013. Sari pia inaaminika kuwa kuwa mhusika, pamoja na Musa Asoglu, kwa mashambulizi ya Machi 2013 dhidi ya Wizara ya Sheria ya Uturuki na makao makuu ya Chama cha Haki na Maendeleo huko Ankara, ambapo mmoja alijeruhiwa.

Musa Asoglu, Zerrin Sari, na Seher Demir Sen ni viongozi muhimu wa Chama cha Mapindizu naUkombozi wa Watu/Front (Kwa Kituruki: Devrimci Halk Kurtuluş Partisi Cephesi, au DHKP/C).

Picha za ziada

Picha zaidi za Zerrin Sari
Picha zaidi za Zerrin Sari