Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Yasin Kilwe

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Yasin Kilwe ni kiongozi wa juu wa al-Shabaab huko Puntland, Kaskazini mwa Somalia. Kama kiongozi wa wapiganaji haramu wa milimani Galgala waishio katika milima ya Golis, Kilwe aliapa utiifu na ushirikiano kwa al-Shabaab na al-Qaida katika taarifa iliyorekodiwa na kusambazwa na kituo cha redio kinachoongozwa na al-Shaab mwishoni mwa Februari 2012. Kiongozi wa ngazi za juu wa al-Shabaa Ahmed Abdi aw-Godane amemteua rasmi Kilwe kama kiongozi wa eneo hilo.

Al-Shabaab ulikuwa ni upepo wa kijeshi wa Halmashauri ya Mahakama ya Kiislamu ya Somalia ambayo ilichukua sehemu kubwa ya Kusini mwa Somalia katika kipindi cha pili cha mwaka 2006. Al-Shabaab imeendeleza vurugu zake za uasi huko Kusini na Katikati ya Somalia. Kundi hili limejitangaza kuhusika kwake na mashambulio mengi ya mabomu – ikiwamo aina za mashambulizi ya utoaji muhanga – ndani ya Mogadishu na Katikati na Kaskazini mwa Somalia, hususani kuwalenga maofisa wa serikali ya Somalia na wale washirika wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG) ya Somalia. Al-Shabaab walikuwa wahusika wa ulipuaji mabomu pacha ya kujitoa muhanga huko Kampala, Uganda mnamo Julai 11, 2010, ambapo watu zaidi ya 70, akiwamo Mmarekani mmoja waliuawa. Kundi hili limewaua wanaharakati wa amani wa Kisomali, wafanyakazi wa kimataifa wa kutoa misaada, watu muhimu katika asasi za kiraia, na waandishi wa habari.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeitaja al-Shabaab kama kundi la kigaidi la nje chini ya kipengele 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia (kama kilivyofanyiwa marekebisho) mnamo Februari 26, 2008, na Kundi la Kigaidi Duniani chini ya Hati Maalum 13224 mnamo Februari 29, 2008. Mnamo Februari 2012, al-Shabaab na al-Qaida walitangaza ushirikiano wao rasmi.