Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Yasin al-Suri

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 10

Ezedin Abdel Aziz Khalil, anayefahamika sana kama Yasin al-Suri, ni mwezeshaji mkuu wa al-Qaida huko Iran. Yasin al-Suri alitiwa mbaroni na mamlaka za Iran mnamo Disemba 2011 baada ya tangazo la dola milioni 10 za zawadi nono za Tuzo za Haki, lakini amechukua tena uongozi wa mtandao wa AQ huko Iran.

Kama mwezeshaji mkuu wa a-Qaida Iran, Yasin al-Suri ana jukumu la kusimamia juhudi za al-Qaida za kuhamisha viongozi na washirika wenye uzoefu kutoka Pakistani kwenda Syria, kuandaa na kudumisha njia ambazo wanachama wapya wanaweza kusafiri kwenda Syria kupitia Uturuki, na kusaidia washirika wa nje hadi Magharibi katika harakati za al-Qaida.

Al-Suri husafirisha fedha na watu wanaokodiwa toka sehemu zote za Mashariki ya Kati kwenda nchini Iran, kasha tena kwenda Pakistani, kusaidia uongozi wa juu wa al-Qaida. Uongozi wa Iran una mahusiano na al-Suri na umemruhusu kufanya shughuli zake ndani ya mipaka ya Iran tangu mwaka 2005.

Al-Suri hushughulikia misafara ya wanaokodiwa kwaajili ya al-Qaida kutoka eneo la Ghuba hadi Pakistani na Afganistani kupitia Iran. Na pia ni mchangishaji wa fedha muhimu wa al-Qaida na amekusanya fedha kutoka kwa wafadhili na wachangishaji wa eneo lote la Ghuba. Al-Suri husambaza kiasi kikubwa cha fedha kupitia Iran kwaajili ya safari zaidi kwenda kwa uongozi wa al-Qaida nchini Afganistani na Iraki.

Huku akifanya kazi na serikali ya Irani, al-Suri hupanga kufunguliwa kwa wanachama wa al-Qaida kutoka jela za Irani. Baada ya kufunguliwa wanachama wa al-Qaida, serikali huwahamishia wanachama hao kwa al-Suri, ambaye hupanga safari zao kuelekea Pakistani.

Picha za ziada

Yasin al-Suri