Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Yahya Haqqani

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Yahya Haqqani ni mwanachama wa ngazi za juu wa Mtandao wa Haqqani ambaye amekuwa akijihusisha katika mambo ya kijeshi, kifedha na propaganda ya kikundi. Yahya amekuwa kiongozi mkuu wa kikundi asiye rasmi pale viongozi wakuu Sirajuddin Haqqani (Shemeji yake na Yahya), Khalil Haqqani na Badruddin Haqqani (marehemu) wanapokuwa hawapo. Yahya amechukua majukumu kama mtunza vifaa wa Mtandao wa Haqqani na amewezesha kufadhiri makamanda wa Haqqani kujumuisha walio ngazi za chini – kwa sasa marehemu Kamanda wa Mtandao wa Haqqani Sangin Zadran na Kiongozi mkuu wa opereshi za kujitoa mhanga, Abdul Rauf Zakir. Yahya pia ameshafanya kazi kama mjumbe na mkalimani wa Kiarabu wa Sirajuddin Haqqani.

Yahya amefanya uwezeshaji mkuu na kusaidia shughuli za mashambulizi ya Mtandao wa Haqqani na shughuli nyinginezo. Mwanzoni mwa 2013, aliwezesha ufadhiri wa wapiganaji wa Mtandao wa Haqqani. Pia mwanzoni mwa 2013, Yahya aliratibu uhamisho wa vifaa kutoka Falme za Kiarabu hadi kwa Kiongozi wa ngazi za juu wa Mtandao wa Haqqani Khalil Haqqani. Mnamo 2012, Yahya aliratibu usambazaji wa vifaa vya milipuko na vifaa vya mawasiliano, na alihakiki maandalizi ya shambulio la Agosti 7, 2012 Mtandao wa Haqqani uliposhambulia Kambi ya Jeshi ya Muungano katika Jimbo la Logar, Afghanistan, ambapo watu kumi na tatu, kujumuisha kumi na moja raia wa Afghanistan, walijeruhiwa. Kuanzia 2011, Yahya alipeleka fedha kutoka kwa Sirajuddin Haqqani kwenda kwa makamanda wa Mtandao wa Haqqani kwa operesheni.

Wakati mwingine Yahya hutumika kama kiungo kati ya Mtandao wa Haqqani na al-Qaida na pia ameendeleza mshikamano huo na al-Qaida walau tangu katikati ya miaka ya 1990. Katika majukumu haya, Yahya ametoa fedha kwa wanachama wa al-Qaida katika ukanda huo kwa matumizi binafsi. Kuanzia katikati ya 2009, alitenda kazi kama kiungo mkuu wa Mtandao wa Haqqani na wapiganaji wa kigeni, ukijumuisha Waarabu, Wauzbeki, na Wachecheni.

Yahya pia aliongoza na kusimamia vyombo vya habari na shughuli za propaganda za Mtandao wa Haqqani na Taliban. Kuanzia mwanzoni mwa 2012, Yahya alikuwa anakutana na Sirajuddin Haqqani kupata dihini ya mwisho kuhusu propaganda za video walizotengeneza. Yahya amefanya shughuli za vyombo vya habari vya Mtandao wa Haqqani kuanzia walau 2009 pale alipofanya mabadiliko kwenye video za wapiganaji huko Afghanistan wakifanya kazi kwenye studio za habari za madrasa za Mtandao wa Haqqani. Kuanzia mwishoni mwa 2011, Yahya alipata fedha kwa ajili gharama za habari za Mtandao wa Haqqani kutoka kwa Sirajuddin Haqqani au mmoja wa watiifu wa Sirajuddin.

Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtambulisha Yahya Haqqani kama Gaidi wa Ulimwenguni kupitia Hati Maalum 13224 mnamo Februari 5, 2014

Picha za ziada

Additional Photo of Yahya Haqqani
Additional Photo of Yahya Haqqani