Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Kupigwa bomu kwa World Trade Center

New York | Februali 26, 1993

Februari 26, 1993, bomu kwenye lori liliripuka chini ya Mnara wa kwanza wa World Trade Center mjini New York. Nia ya kutega bomu hilo la paundi 1,500 ilikuwa ni kuharibu majengo yote mawili kwa kufanya mnara wa kwanza uangukie mnara wa pili, na kuua maelfu ya watu. Ingawa mlipuko haukuharibu minara ya jengo hilo, uliua watu sita na kujeruhi zaidi ya elfu moja, na kusababisha uharibifu wa mamia ya mamilioni ya dola.

Shambulizi lilipangwa na kundi la watu wenye uhusiano na al-Qaida akiwemo Abdul Rahman Yasin, Ramzi Yousef, na wengine kadhaa. Ufadhili kwa operesheni hii ulitolewa na Khalid Shaikh Mohammed, mjomba wa Ramzi Yousef na mwanachama wa juu wa al-Qaida. Wanaume wengine sita waliohusika na shambulizi hili wamehukumiwa, akiwemo mpangaji mkuu, Ramzi Yousef.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.