Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki anatafutwa kuhusiana na utekaji nyara wa ndege Septemba 5, 1986 ya Pan Am 73 ikiwa ardhini mjini Karachi, Pakistan. Mtu huyo aliyetajwa hapo juu amefunguliwa mashtaka yafuatayo:

Njama za kufanya uhalifu dhidi ya Marekani; njama za kuwaua raia wa Marekani nje ya Marekani; mauaji ya raia wa Marekani nje ya Marekani; jaribio la kuwaua raia wa Marekani nje ya Marekani; kusababisha madhara makubwa ya kimwili kwa raia wa Marekani nje ya Marekani; utekaji nyara; kutumia silaha wakati wa kitendo cha uhalifu cha kutumia nguvu; kuweka vifaa vya uharibifu kwenye ndege; kufanya kitendo cha kutumia nguvu dhidi ya mtu kwenye ndege; uharamia wa ndege; uharibifu wa nia mbaya kwenye ndege; na kusaidia na kuwezesha uhalifu.

Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki, Jamal Saeed Abdul Rahim, Muhammad Abdullah Khalil Hussain ar-Rahayyal, na Muhammad Ahmed al-Munawar wamefunguliwa mashtaka katika mahakama ya District of Columbia kwa jukumu lao katika utekaji nyara wa ndege ya Pan Am 73 tarehe 5 Septemba, 1986 ikiwa ardhini mjini Karachi, Pakistan. Baada ya kuishikilia ndege na abiria wake na wafanyakazi 379, wakiwemo raia wa marekani wasiopungua 78, kwa karibu saa 16, watekaji nyara walianza kushambulia abiria kiholela, na kusababisha vifo vya abiria wasiopungua 20 na kujeruhi vibaya wengine zaidi ya 100. Watu hawa wanaaminika kuwa wafuasi wa Shirika la Abu Nidal, shirika la mfumo wa magaidi wa kimataifa.

Picha zaidi za

Picha ya Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki