Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Shambulizi kwenye meli ya kijeshi USS Cole

Aden, Yemen | Oktoba 12, 2000

Asubuhi ya Septemba 11, 2001, magaidi 19 wenye uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaida waliteka nyara ndege nne za abiria. Ndege hizi zilikuwa zinaelekea California, zikitokea kwenye viwanja tofauti vya ndege mashariki mwa Marekani.

Ndege mbili za kwanza ziliondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Logan huko Boston, zilitekwa, na kugonga minara muhimu ya World Trade Center mjini New York. Mshtuko wa ndege hizi, na moto mkubwa wa mafuta ya ndege, uliharibu kabisa jengo na kusababisha jengo kuporomoka.

Ndege ya tatu iliondoka uwanja wa kimataifa wa Dulles, ilitekwa, na kugonga jengo la Pentagon nusu saa tu baada ya jengo la World Trade Center kushambuliwa kwa mara ya pili. Shambulizi hilo liliharibu vibaya sehemu kubwa ya jengo, na kuua abiria wote waliokuwa ndani na watu wengine 125 waliokuwa ndani ya jengo.

Ndege ya nne iliondoka uwanja wa kimataifa wa Newark na kwa hakika ilikuwa ikielekea kwenye jengo la bunge la Marekani au Ikulu ya Marekani, White House. Hata hivyo, abiria waliokuwa ndani ya ndege walipambana na magaidi kugombea udhibiti wa ndege. Kwa sababu ya ushujaa wa raia hawa, magaidi hawakufanikiwa kutekeleza lengo lao na ndege ilianguka karibu na Shanksville, Pennsylvania, na kuua watu wote 40 waliokuwa ndani ya ndege.

Mashambulizi ya Septemba 11, 2001, yaliua raia 2,998 kutoka nchi mbali mbali kote ulimwenguni. Mtandao wa kigaidi wa al-Qaida ulidai kuhusika katika kupanga na kutekeleza mashambulizi haya, na kiongozi wao, ambaye sasa ni marehemu,Usama bin Ladin, alikiri kuwajibika katika ujumbe wake kwenye kanda ya video kufuatia mashambulizi hayo. Haya yalikuwa mashambulizi ya kutisha sana nchini Marekani kufanywa na kundi la nje tangu shambulizi la Pearl Harbor mwaka 1941.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni 25 kwa taarifa itakayopelekea kuwafikisha mbele ya sheria wale waliohusika na mashambulizi haya.