Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Ndege ya TWA 847 ilitekwa

Beirut, Lebanon | Juni 14, 1985

Juni 14, 1985, magaidi wenye uhusiano na Hezbollah waliiteka ndege TWA 847, ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Athens, Ugiriki kwenda Roma, Italia. Magaidi kwanza waliibadili safari ya ndege hiyo na kuelekea Beirut, Lebanon, ambako abiria kadhaa waliachiliwa kwa mabadilishano ya mafuta. Ndege baadae iliondoka kuelekea Algiers, Algeria, ambako abiria zaidi waliachiliwa kabla ya ndege kurejea Beirut.

Huko Beirut, magaidi walimtambua mzamiaji wa jeshi la majini la Marekani Robert Stethem. Magaidi walimshambulia na kumpiga risasi Stethem, baadae kuutupa mwili wake barabarani. Mjini Beirut, watu zaidi ya 12 wenye silaha waliingia ndani ya ndege kabla ya kurejea Algiers, ambako abiria 65 zaidi waliachiliwa.

Hatimaye, ndege ilirejea tena Beirut, ambako ilibakia huko hadi Juni 30, ambapo abiria waliobaki walipelekwa Syria. Nchini Syria, walipanda ndege ya jeshi la anga la Marekani na kusafirishwa hadi Ujerumani. Magaidi waliohusika na shambulizi hili ni pamoja na Ali Atwa, Hasan Izz-al-Din, Mohammed Ali Hamadei na wengine kadhaa.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.