Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Usafirishaji wa mafuta na mambo ya kale kulinufaisha Taifa la Kiislamu la Iraq na Levant (ISIL)

Mpango wa Tuzo za Haki unatoa zawadi nono hadi kufikia dola milioni 5 kwa taarifa inayopelekea uzuizi mkubwa wa mauzo na/au biashara ya mafuta na mabo ya kale ufanywao na, kwa au kwa niaba kunufaisha kikundi cha kigaidi cha Dola ya Kiislam ya Iraq na Levant (ISIL), ambalo pia hufaamika kwa kifupi chake kwa Kiarabu kama DAESH.

Makundi ya kigaidi kama ISIL yanategemea ufadhili na msaada wa kimtandao kuhimili operesheni na kufanya mashambulizi. Operesheni haramu ya mafuta na mambo ya kale ya ISIL ni ya uporaji vifaa vya kale kutoka Syria na Iraq ni vyanzo muhimu vya mapato, kusaidia makundi ya kigaidi kujipatia mamilioni ya dola kwa fedha taslimu na kuwezesha ISIL kuendesha mbinu zao za kikatili na uonevu kwa raia wasio na hatia. Uharibifu wa ISIL na uporaji vifaa vya kiutamaduni na kihistoria katika Iraq na Syria umeharibu ushahidi wa maisha ya kale na jamii isiyoweza kurudishwa tena. Sarafu za Kale na za kihistoria, kujitia (vitengenezavyo na sonara) na vito vya kuchonga, picha za kuchora za ukutani, vinyago, vyombo, na vidonge aina ya cuneiform ni miongoni mwa aina ya vitu vya kiutamaduni kutoka Syria na Iraq ambavyo ISIL inavitafuta. Orodha ya Dharura ya vitu vyekundu vya kitamaduni vilivyo katika hatari (hatarini), iliyoandaliwa na Baraza la Kimataifa la Makumbusho kupitia msaada wa Idara ya Nchi wa Marekani, imetoa orodha ya kina ya aina ya vitu vilivyoporwa na kuuzwa kutoka Syria na Iraq, http://icom.museum/resources/red-lists-database/red-list/syria/ na http://icom.museum/resources/red-lists-database/red-list/iraq-2015/

Kwa lengo la kukabiliana na ufadhili wa ISIL, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inaamini zawadi nono hii itazalisha taarifa kuhusiana na watu au taasis zinazohusika na uzalishaji, uwezeshaji, usindikaji, magendo, usambazaji, uuzaji, na biashara ya mafuta na mambo ya kale ambayo hunufaisha ISIL, pamoja na taarifa kuhusiana na mitandao ya magendo, mbinu, na njia za msingi za shughuli hizi.

http://eca.state.gov/video/conflict-antiquities-panel-1-video

http://eca.state.gov/video/conflict-antiquities-panel-2-video

Mambo ya Kale

Mambo ya Kale
Mambo ya Kale
Mambo ya Kale
Mambo ya Kale
Mambo ya Kale
Mambo ya Kale