Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Mauaji katika kituo cha Petroli cha Union Texas 

Karachi, Pakistan | Novemba 12, 1997

Asubuhi ya Novemba 12, 1997, wafanyakazi wanne wa kampuni ya Union Texas Petroleum (UTP) walikuwa njiani kuelekea kazini mjini Karachi, Pakistan. Wakati gari yao ilipokuwa inavuka daraja, watu wawili wenye bunduki walitoka kwenye gari jekundu, Honda Civic na kuifyatulia risasi gari yao. Wafanyakazi wanne wote raia wa Marekani, pamoja na dereva wao Mpakistan, waliuawa katika shambulizi.

Wachambuzi wengi wanaona mashambulizi kuwa ni kisasi kwa kuhukumiwa kwa Mir Aimal Kansi siku mbili awali, ingawaje dhana hiyo haijawahi kuthibitishwa rasmi. Kansi alipatikana na hatia ya mauaji ya mwaka 1993 ya wafanyakazi wawili wa CIA nje ya makao makuu ya idara hiyo huko Langley, Virginia.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.

Waathirika

Picha ya Ephrahim Egbu
Ephrahim Egbu
Picha ya Joel Enlow
Joel Enlow
Picha ya Tracy Ritchie
Tracy Ritchie
Picha ya William Jennings
William Jennings