Habari za ushuhuda wa Mafanikio

Ramzi Ahmed Yousef

Aliyepatikana na Hatia

Ramzi Ahmed Yousef alikuwa mpangaji mkuu wa ugaidi aliyehusika na ulipuaji bomu wa Februari 1993 kwenye jengo la World Trade Center mjini New York ambapo watu sita waliuawa na wengine zaidi ya elfu moja walijeruhiwa. Yousef na wasaidizi wake waliendesha gari lililojaa milipuko katika eneo la chini kwenye jengo la World Trade Center. Katika muda wa saa chache za ulipuaji bomu, Yousef aliondoka na ndege kuelekea Pakistan.

Yousef aliibukia nchini Phillipines ambako alijihusisha katika kuendeleza njama za kigaidi. Yousef alipanga kumuua Baba Mtakatifu Yohana Paulo wa pili Januari 14, 1995 wakati alipokuwa akitembelea Phillipines, na kulipua ndege 12 za Kimarekani huko Asia siku chache baadae. Kwa ujumla njama hiyo ilijulikana kama “Oplan Bojinka,” neno ambalo tafsiri yake kwa lugha isiyo rasmi ya Kiarabu ina maana “Operesheni ya Mlipuko” au Operesheni ya Mtikisiko mkubwa”. Yousef alikuwa mpanganji mkuu aliyehusika na Oplan Bojinka, lakini wahusika wengine wakuu katika Oplan Bojinka ni pamoja na Wali Khan Amin Shah, Abdul Hakim Murad, Khalid Shaikh Mohammad (mjomba wake Yousef na mpangaji mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11), na Hambali – wote wanachama wa Al Qaida.

Kama sehemu ya njama ya jumla, hapo Januari 21 na 22, 1995, magaidi watano walikuwa watege mabomu kwenye ndege 12 zilizokuwa zinaelekea Marekani baada ya kutua huko Asia Mashariki na Kusini Mashariki wakati wa safari ya kwanza ya kila ndege na baadae kuondoka kabla ya ndege hizo kulipuka sambamba juu ya Bahari ya Pasifiki. Kila mmoja wa magaidi watano walikuwa wamepewa jukumu la kupanda ndege mara mbili au hata mara tatu mpaka ndege zote 12 ziwekewe mabomu ndani. Idadi iliyofikiriwa ya vifo katika mpango wa awamu hii ilikuwa zaidi ya watu elfu nne.

Bahati nzuri, Yosef na washirika wake walikuwa wazembe kiasi, na hivyo ikageuka kuwa ndiyo mwisho wao. Januari 6, 1995, Yousef na Murad walilazimika kukimbia nyumbani kwao mjini Manila wakati mchanganyiko wa kemikali ulipoleta moshi mkubwa, na kumiminika nje ya dirisha la nyumba yao. Yousef alimtaka Murad kurejea ndani ya jengo kuondoa kompyuta na ushahidi mwingine wa kuwatia hatiani. Wakati Murad aliporejea nyumbani , hata hivyo, alikutana na polisi ambao tayari walikuwa wamewasili katika eneo hilo. Yousef, alibaini kwamba Murad lazima amekamatwa, na hivyo alikimbilia Pakistan.

Mwezi Februari 1995, mtoa habari, aliona kijitabu cha RFJ na kushawishika na tuzo inayotolewa, alikwenda ubalozi wa Marekani mjini Islamabad, Pakistan na kutoa habari zilizowezesha kufahamika sehemu ambako Yousef alikuwepo. Februari 7, 1995, mamlaka za Pakistan, wakisaidiana na mawakala wa Ulinzi wa kidiplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje walimkamata Yousef mjini Islamabad, Pakistan, na kumpeleka nchini Marekani. Yousef hivi sasa yuko gerezani huko Colorado. Washirika wengine wanne waliohusika na Oplan Bojinka pia wamekamatwa.