Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Radullan Sahiron

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 1

Radullan Sahiron ni kiongozi mwandamizi wa kundi la Abu Sayyaf (ASG) lenye makao yake Ufilipino. Kundi hilo lilijitenga kutoka kundi kubwa zaidi la Moro National Liberation Front mwanzoni mwa miaka ya 1990 chini ya uongozi wa Abdurajak Abubakar Janjalani, ambaye aliuawa katika mapambano na polisi wa Ufilipino mwezi Desemba 1998. Mdogo wake, Khadaffy Janjalani, alimrithi kama kiongozi wa kundi hilo. Mwezi Septemba 2006, Khadaffy Janjalani aliuawa katika mapambano ya bunduki na jeshi la Ufilipino. Radullan Sahiron anadhaniwa kuwa kiongozi mpya wa ASG.

Watu wengi wasio na hatia, wanaume, wanawake na watoto wamekufa au kujeruhiwa vibaya kutokana na vitendo vya Sahiron. Sahiron alikuwa na jukumu katika utekaji nyara wa raia watatu wa Marekani Mei 2001 huko Dos Palmas, wakiwemo Martin na Gracia Burnham, na raia 17 wa Ufilipino kutoka eneo la mapumziko la watalii la Palawan, Ufilipino. Baadhi ya mateka, akiwemo raia wa Marekani Guillermo Sobero, waliuawa.

Sahiron anaaminika kuwa amejificha katika eneo la kusini la Mindanao ambako anaendelea kupanga njama za ugaidi ambazo zimeathiri jumuiya nyingi. Kwa sababu ya nafasi yake ya uongozi ndani ya ASG, kundi ambalo mashambulizi yake ya kigaidi yamesababisha vifo vya raia wa Marekani na Ufilipino, wakuu wa Marekani wanamwona Sahiron kuwa kitisho kwa raia na maslahi ya Marekani na Ufilipino.

Sahiron amepoteza mkono wake wa kulia katika mapigano na majeshi ya usalama katika miaka ya 1970. Anazungumza Kiarabu na Kitausug.