Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Utekaji nyara wa ndege ya Pan Am 73

Karachi, Pakistan | Septemba 5, 1986

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeidhinisha zawadi ya dola zifikiazo milioni $5 kila mmoja kwa habari zitakazopelekea kukamatwa na/au kufikishwa hatiani kwa Wadoud Mohammad Hafiz-al Turki, Jamal Saeed Abdul Rahim, Mohammad Abdullah Khakil Hussain ar-Rahayyal, na Muhammad Ahmed al-Munawar—wote wakiaminika kuwa wafuasi hapo awali wa kundi la kigaidi la Abu Nidal.

Wakati ilipokuwa ardhini mjini Karachi, Pakistan, ndege ya Pan Am 73 ilitekwa nyara inakadiriwa saa kumi na mbili asubuhi tarehe 5 Septemba, 1986 na wafuasi wa kundi la Abu Nidal. Abiria 379 na wafanyikazi wa ndege, kukiwemo raia wa Marekani wasiopungua 78, walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ilipotekwa nyara. Wafanyikazi wa ndege walitoroka, wakiacha ndege bila jinsi. Watekaji nyara waliikamata ndege na kuanza kudai wafanyikazi wa ndege na marubani waiendeshe ndege pamoja na abiria wake hadi Cyprus. Wakati wa utekaji nyara, raia mmoja wa Marekani aliuawa katika mlango wa ndege. Katika mwisho wa kitendo cha utekaji nyara, watekaji waliwashambulia abiria. Abiria wasiopungua 20 waliuawa, na zaidi ya 100 kujeruhiwa vibaya.

Wakuu wa Pakistan walikamata watuhumiwa wanne katika eneo la tukio na baadaye wakamkamata mtu wa tano aliyesaidia kupanga shambulizi. Wote watano, wakiwemo na wanne ambao wanazungumziwa katika toleo hili la zawadi, walishtakiwa, na kukutwa na hatia na kufungwa jela nchini Pakistan.

Septemba mwaka 2001, Zayd Hassan Abd al-Latif Safarini, mmoja kati ya magaidi waliokutwa na hatia, aliachiliwa baadaye na wakuu wa Pakistan. Alikamatwa hatimaye na FBI na kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya serikali kuu Marekani. Desemba 16, 2003, Safarini alikubali kuafikiana mahakama na Wizara ya Sheria ya Marekani. Tarehe 13 Mei, alihukumiwa kifungo cha miaka 160 jela.

Mwezi Januari 2008, watekaji nyara wanne ambao wanatajwa katika zawadi hii inasemekana waliachiwa huru nchini Pakistan. Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki, Jamal Saeed Abdul Rahim, Muhammad Abdullah Khalik Hussain ar-Rahayyal, na Muhammad Ahmed al-Munawar wamefunguliwa mashtaka katika mahakama ya District of Columbia kwa jukumu lao katika utekaji nyara huo na bado hawajakamatwa.

Kwa maelezo zaidi, angalia Wanatafutwa kwa Ugaidi

Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki

Muhammad Ahmed al-Munawar

Muhammad Abdullah Khalil Husaain ar-Rahayyal

Jamal Saeed Abdul Rahim