Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Musa Asoglu

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Musa Asoglu ni kiongozi muhimu wa Chama cha Mapinduzi na Ukombozi wa Watu/Front (Kwa Kituruki: Devrimci Halk Kurtuluş Partisi Cephesi, au DHKP/C). DHKP/C ililenga maslahi ya Marekani, ikijumuisha majeshi ya Marekani na wafanyakazi wa kibalozi pamoja majengo ya kibalozi tangu kuundwa kwake mnamo mwaka 1994 pale kundi tangulizi lake, Devinmci Sol au Dev Sol, lilipogawanyika. Lengo lake ni kutokomeza nyayo za Marekano na NATO toka Uturuki, na kujenga taifa la kijamaa. Mnamo Februari 2013, mtoaji mhanga wa bomu aliyehusishwa na kikundi hiki alishambulia ubalozi wa Marekani huko Ankara, kuua mlinzi wa kituruki. Serikali ya Mambo ya Nje iliitanza DHKP/C kuwa ni kundi la nje ya kigaidi tangu mwaka 1997, na kupitiwa upya na kufikiwa kwa hitimisho hilohilo tena mnamo Julai 24, 2013.

Musa Asoglu alijiunga na DHKP/C mnamo miaka ya 1990 wakati alipokuwa mkazi wa Uholanzi. Aliripotiwa kuwa mrithi wa uongozi wa kundi hili baada ya kiongozi mhasisi wa kundi hili, Dursun Karatas, kufariki mnamo mwaka 2008. Asoglu ni kiongozi wa kamati kuu ya DHKP/C, ambayo ni ngazi ya juu kabisa ya kamati ya maamuzi, na inaamina kuwa inaongoza masuala yote ya kifedha na shughuli za uchangishaji huko Ulaya. Aliripotiwa kuamuru mauaji ya kujitoa mhanga kwa bomu katika ubalozi wa Marekani mjini Ankara mnamo Februari 1, 2013, ambalo liliua mlinzi mmoja raia wa Uturuki. Pia inaaminika kuwa alikuwa ni mhusika wa mamshambulizi mnamo Machi 2013 dhidi ya makao makuu ya Chama cha Haki na Maendeleo (AKP) na Wizara ya Sheria ya Uturiki.

Musa Asoglu, Zerrin Sari, na Seher Demir Sen ni viongozi muhimu wa Chama cha Mapindizu naUkombozi wa Watu/Front (Kwa Kituruki: Devrimci Halk Kurtuluş Partisi Cephesi, au DHKP/C).

Picha za ziada

Picha zaidi za Musa Asoglu
Picha zaidi za Musa Asoglu
Picha zaidi za Musa Asoglu