Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Mohamed Makawi Ibrahim Mohamed

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Mnamo Januari 1, 2008, raia wa Marekani na mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Kimataifa (USAID) John Granville na dereva wake raia wa Sudan, Abdelrahman Abbas Rahama, walipigwa risasi na kufariki dunia wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwao wakitokea kwenye mkesha wa kuuaga mwaka mjini Khartoum, Sudan.  Makundi mawili kwa nyakati tofauti yalijitangaza na kutamba kuwa ni wahusika wa shambulio la mauaji.  Kwa sasa kundi la al-Qaida katika Ardhi ya Mito Miwili ya Nile (AQTN) na Ansar al-Tawhid (Waunga mkono wa itikadi yauwepo wa Mungu mmoja pekee – Monotheism).

Watu watano walishitakiwa na kutkutwa na hatia katika mamlaka ya mfumo wa sheria za Sudan kwa ushiriki wao katika mauaji.  Abdelraouf Abu Zaid Mohamed Hamza, Mohamed Makawi Ibrahim Mohamed, Abdelbasit Alhaj Alhassan Haj Hamad, na Mohanad Osman Yousif Mohamed walihukumiwa kifo cha kunyongwa, lakini walitoroka katika gereza la Khober la mji wa Khartoum mwaka mmoja baada ya hukumu yao.  Mohanad aliripotiwa kufariki mnamo Mei, 2011.  Abdelraouf alikamatwa tena na mamlaka ya Sudan.  Makawi na Abdelbasit bado hawajakamatwa.

Makawi alikuwa na ushirikiano na kundi la Sudan lifahamikalo kama al-Qaida Katika Ardhi ya mito miwili ya Nile, ambalo lilipanga kuishambulia Marekani, nchi zingine za Magharibi na maslahi ya Sudan.  Alikuwa kiongozi wa kundi ambalo lilitekeleza shambulizi la Januari 1, 2008, na alitambuliwa kama mmoja wa washambuliaji wawili katika mauaji.  Baada ya kutoroka katika gereza la Khobar mjini Khartoum manamo Juni 11, 2010, Makawi alikwenda Somalia.