Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Kupigwa bomu kwa kambi ya jeshi Kikosi cha maji

Lebanon | Oktoba 23, 1983

Mwezi Oktoba 23, 1983, bomu kwenye lori lililipuka katika eneo la makazi ya wanajeshi wa kimataifa wa Marekani na Ufaransa nchini Lebanon. Shambulizi liliua mamia ya wanajeshi, wakiwemo Marine 241 wa Marekani. Jeshi mchanganyiko lilikuwa nchini Lebanon kama sehemu ya juhudi za kimataifa za ulinzi wa amani. Hezbollah inaaminika walipanga shambulizi hilo, wakipata msaada na ufadhili kutoka Iran.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni Tano kwa taarifa itakayopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na mashambulizi haya.