Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Malik Abou Abdelkarim

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Malik Abou Abdelkarim ni kiongozi wa juu wa kikundi cha wapiganaji ndani ya kundi la kigaidi, al-Qaida katika Ardhi ya Kiislamu ya Maghreb (AQIM).  Chini ya utawala wa Abdlkarim, kikundi chake kilipata silaha na kufanya utekaji nyara na mashambulizi yasiyo makubwa huko Kaskazini na Magharibi mwa Afrika.  Abdelkarim aliripotiwa kuwa mhusika wa mauaji ya mateka wa Kifaransa mwenye umri wa miaka sabini na nane huko Niger mnamo Julai 2010.  Shambulio la Juni 2010 lililofanywa na kikundi cha Abdelkarim lilisababisha vifo vya askari 11 wa Kialjeria.

Kundi la al-Qaida katika Ardhi ya Kiislamu ya Maghreb (AQIM), hapo awali lilifahamika kama Kundi la Sala, mahubiri na mapambano (GSPC), lilifanya zaidi ya dazeni ya mashambulizi ya kigaidi katika maeneo ya Kaskazini magharibi mwa Afrika.  AQIM lilitamba na kutangaza uhusika wake wa mabomu ya kujitoa muhanga, utekaji nyara wa watu wa Magharibi, mauaji, na mashambulizi ya milipuko.Kundi hilo lilifanya kwa wakati mmoja mashambulizi mawili mnamo Disemba 2007, kushambulia makao makuu ya Umoja wa Mataifa na Baraza la Katiba la Algeria, na kuua watu 42 na kujeruhi 158.  AQIM pia walitamba kuhusika na mauaji ya Juni 2009 ya raia wa Marekani Christopher Legget, ambaye alikuwa huko Mauritania kwa shughuli za kidini.  Mnamo Septemba 2012, AQIM iliwahamasisha wanachama wake kuwatisha Balozi za Marekani na kuua mabalozi wa Marekani.  AQIM ilitangaza rasmi uhusiano wake na al-Qaida mnamo Septemba 2006, na tangu hapo imethibitisha lengo lake la kufanya mashambulizi kwa Magharibi.

Serikali ya Mambo ya Ndani ya Marekani iliitangaza GSPC kama Kundi la Nje la Kigaidi chini ya Sehemu ya Kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia (kama kilivyorekebishwa) mnamo Machi 27, 2002, na kuunda upya wajibu wake chini ya jina jipya la AQIM mnamo Oktoba 16, 2009.  Wizara ya Fedha ya Marekani ililitangaza kikundi kama Kikundi Rasmi cha Kigaidi chini ya Hati Maalumu 13224 mnamo Februari 21, 2008.