Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Maalim Salman

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Maalim Salman alichaguliwa na kiongozi wa al-Shabab ambaye ni marehemu sasa, Ahmed Abdi aw-Mohamed (Godane) kuwa mkuu wa wapiganaji wa kiegni wa Afrika kwa ajili ya al-Shabaab. Amewafundisha magaidi wa al-Shabaab ambao sio wasomali na amekuwa anahusika katika operesheni barani Afrika kuwalenga watalii, sehemu za starehe, na makanisa.

Japokuwa alikuwa amejikita zaidi kwenye operesheni nje ya Somalia, Salman anafahamika kuishi Somalia na kuwafundisha wapiganaji wa kigeni nchini Somalia kabla ya kuwatawanya sehemu zingine. Miongoni mwa mashambili mengineyo ya kigaidi, al-shabaab walihusika kwa shambulio la Septemba 2013 la Maduka ya Westgate, Kenya ambalo liliacha walau watu 65 kufariki.