Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Kadhia ya barua zilizokuwa na bomu

Desemba 1996 mpaka Januari 1997


Kati ya Desemba 1996 na Januari 1997, barua 16 zilizokuwa na mabomu ambazo zikipachikwa kama kadi za sikukuu zilipelekwa kwa njia ya posta kwa watu mbali mbali nchini Marekani na Uingereza.

Kati ya barua hizi zilizokuwa na mabomu, 13 zilifika kwenye ofisi za gazeti la Al Hayat mjini New York, Washington, D.C., na London. Bomu moja lililipuka mjini London, na kujeruhi vibaya sana watu wawili wasiokuwa na hatia. Barua nyingine tatu zenye mabomu ziligundulika Marekani katika gereza la serikali kuu huko Leavenworth, Kansas.

Kila barua iliyokuwa na bomu ilikuwa na muhuri wa Alexandria, Misri na tarehe ilikuwa Desemba 21, 1996, na hakuna iliyokuwa na anwani ya ilipotoka. Mabomu yalikuwa katika bahasha nyeupe, huku anwani zikiwa zimechapwa kwa kompyuta na zikiwa na alama nyingine mbali mbali.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni Tano kwa taarifa itakayopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na mashambulizi haya.

Picha zaidi za

Kadhia ya barua zilizokuwa na bomu