Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Utekaji nyara na Mauaji

Lebanon | 1985 mpaka 1989

Utekaji nyara kadhaa na mauaji yalikuwa sehemu ya muongo mzima wa mzozo wa utekaji nyara huko Lebanon uliofanywa na magaidi wenye uhusiano na Hezbollah. Mzozo wa utekaji nyara ulidumu kuanzia mwaka 1982 mpaka 1992.

Machi 16, 1984, magaidi walimteka nyara William Buckley, mkuu wa kitengo cha CIA mjini Beirut. Buckley alihojiwa, aliteswa na kushikiliwa mateka kwa miezi 15 kabla ya tarehe inayokisiwa ya kifo chake.

Desemba 3, 1984, mkutubu katika Chuo Kikuu cha Marekani mjini Beirut, Peter Kilburn aliripotiwa kupotea. Miezi 16 baadae, yeye na mateka wenzake wawili walipigwa risasi na kuuliwa, miili yao ilitupwa eneo la milimani mashariki mwa Beirut.

Februari 17, 1988, magaidi walimteka Kanali Willian Higgins kutoka katika gari la ulinzi wa amani la Umoja Mataifa. Alipokuwa mateka Kanali Higgins alihojiwa na kuteswa kabla ya kuuawa. Tarehe kamili ya kifo chake haijulikani.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni Tano kwa taarifa itakayopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na mashambulizi haya.

Waathirika

Picha ya William Higgins
William Higgins
Picha ya Peter Kilburn
Peter Kilburn
Picha ya William Buckley
William Buckley