Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Kupigwa bomu kwa Khobar Towers

Dhahran, Saudi Arabia | Juni 25, 1996

Juni 25, 1996, wanachama wa Hezbollah ya Saudia Arabia walifanya shambulizi la kigaidi kwenye jengo la Khobar Towers, eneo la makazi karibu na Dhahran, Saudia Arabia. Wakati huo, jengo hilo lilikuwa likitumiwa kama makazi ya wanajeshi wa Marekani. Muda mfupi baada ya kuendesha gari la kubeba petroli lililojaa milipuko ya plastiki katika sehemu ya kuegeshea magari katika eneo hilo, magaidi walilipua mabomu, wakiharibu majengo yote ya karibu. Shambulo liliua wanajeshi 19 wa Marekani na raia mmoja wa Saudia Arabia, na kujeruhi wengine 372 kutoka mataifa mbali mbali.

Juni 21, 2001, jopo la mahakama huko Alexandria, Virginia, liliwakuta na hatia magaidi 14 kwa shambulio. Mashtaka yanawataja Ahmad al-Mughassil, Ali el-Hoorie, Ibrahim al-Yacoud, Abdelkarim al-Nasser, na wengine kadhaa kwa hatia mbalimbali za kihalifu. Kwa mujibu wa mashtaka, tisa kati ya magaidi 14 wameshtakiwa kwa makosa 46 tofauti ya kihalifu, ikiwemo yafuatayo: njama za kuwaua Wamarekani na wafanyakazi wa Serikali ya Marekani, kutumia silaha za maangamizi, na kuharibu mali za Marekani; kulipua mabomu; na mauaji.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.