Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Khalil Haqqani

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Mwanachama wa ngazi za juu wa Mtandao wa Haqqani, Khalil al-Rahman Haqqani anashiriki katika harambee mbalimbali za kukusanya fedha kwa niaba ya Taliban na kutoa msaada kwa Taliban wanaondesha shughuli zao Afghanistan. Mwanzoni mwa mwaka 2010, alitoa fedha kwa kambi za Taliban katika Jimbo la Logar, Afghanistan. Mnamo 2009, Khalil alikuwa miongoni mwa waliohusika na kuwaweka kizuizini mateka wote waliokamatwa na Taliban na Mtandao wa Haqqani. Khalil alipokea amri za operesheni za Taliban toka kwa mpwa wake Sirajuddin Haqqani, ambaye alishabainishwa na Marekani mnamo Machi 2008 kwa mujibu wa Hati Maalum 13224. Pia Khalil alifanya kazi kwa niaba ya al-Qaida na amekuwa akihusishwa na operesheni za kijeshi za al-Qaida. Mnamo 2002, alikuwa anasafirisha wanaume kuimarisha mambo ya al-Qaida katika jimbo la Paktia, Afghanistan.

Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtambulisha Khalil al-Rahman Haqqani kama Gaidi wa Ulimwenguni kupitia Hati Maalum 13224 mnamo Februari 9, 2011

Picha za ziada

Picha zaidi za Khalil Haqqani
Picha zaidi za Khalil Haqqani