Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Mabomu kwenye balozi za Marekani

Kenya na Tanzania | Agosti 7, 1998

Mnamo Agosti 7, 1998, wanachama wa kikundi cha kigaidi cha al-Qa’ida kwa wakati huo huo walipiga mabomu kwenye Ubalozi wa Marekani Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania. Programu ya Haki inatoa zawadi ya hadi dola milioni 5 kwa habari ambayo italeta haki kwa mtu yeyote ambaye alihusika na mashambulizi haya.

Ndani ya Nairobi, magaidi wakiendesha lori lililobeba mabomu walilipua bomu kubwa karibu na gereji ya maegesho ya ubalozi wa Marekani, na kuua watu 213, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi 44 wa ubalozi (Wamarekani 12 na watu 32 wa kigeni), na kuumiza wengine zaidi ya 5,000, ikiwa ni pamoja na Balozi wa Marekani Prudence Bushnell

Dar es Salaam, magaidi wakiendesha gari lenye kubeba mabomu walijaribu kugonga lango/geti la ubalozi, wakaanza kupiga risasi kwenye ukumbi, na kisha kulipua mabomu yao. Mlipuko huo uliua watu 11 na kujeruhiwa 85.

Mabomu hayo yalisababisha uharibifu mkubwa wa majengo ya ubalozi na kuharibu ofisi za biashara zilizo karibu.

 

Watu wafuatayo walifunguliwa mashtaka na kuhukumiwa katika mahakama ya shirikisho la Marekani kuhusiana na mashambulizi:  
  • Mamdouh Mahmud Salim, mwanachama mwanzilishi wa al-Qaida, alikamatwa mnamo Septemba 1998 nchini Ujerumani na akaondolewa. Anatumikia hukumu ya maisha katika jela ya shirikisho kwa kuhusika kwake na mabomu.
  • Mnamo Oktoba 2001, Waendeshaji wa al-Qaida, Wajh El-Hage, Khalfan Khamis Mohamed, Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali, na Mohamed Sadeek Odeh walihukumiwa kwa kupanga na kutekeleza ulipuaji wa mabomu ubalozini na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
  • Mnamo Januari 2011, mwendeshaji wa al-Qaida Ahmed Khalfan Ghailani alipatikana n hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama ya Marekani kwa jukumu lake katika mabomu.  
  • Mnamo Septemba 2014, Adel Abdel Bari, kiongozi wa karibu wa kiongozi wa al-Qaida, Zawahiri, alikubali kuwa na hatia ya kuua watu wa Marekani na kuhukumiwa  miaka 25 na mahakama ya shirikisho.
  • Mnamo Mei 2015, Khaled al-Fawwaz, naibu wa Usama Bin Laden, alihukumiwa kufungwa jela na mahakama ya shirikisho kwa kuunganishwa kwake na mashambulizi hayo.
Watuhumiwa wafuatayo walifunguliwa mashtaka kwa mabomu na juri kuu ya shirikisho la Marekani:  

Ayman al-Zawahiri, kiongozi wa sasa wa al-Qaida

Sayf al-Adl, kiongozi muhimu wa al-Qai’da

Abdullah Ahmed Abdullah, kiongozi muhimu wa Qai’da

Usama bin Laden, kiongozi wa zamani wa al-Qaida (Marehemu)

Mohammed Atef, kiongozi wa zamani wa kijeshi wa al-Qaida (Marehemu)

Anas al-Libi, kiongozi wa zamani wa al-Qaida (Marehemu)

Programu ya Tuzo ya Haki inatoa zawadi ya hadi dola milioni 10 kila mmoja kwa taarifa itakayopelekea kufahamu mahali, kukamatwa, au kupatikana na hatia kwa Sayf al-Adl na Abdullah Ahmed Abdullah, na malipo ya hadi dola milioni 25 kwa habari juu ya Ayman al-Zawahiri.
 

Zawadi inatolewa kuhusiana na mabomu ya ubalozi wa Marekani

Ayman Zawahiri

Abdullah Ahmed Abdullah

Sayf al-Adl

Picha zaidi za

English East Africa Bombing PDF
Picha ya Mabomu kwenye balozi za Marekani
Picha ya Mabomu kwenye balozi za Marekani
Picha ya Mabomu kwenye balozi za Marekani
Picha ya Mabomu kwenye balozi za Marekani