Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Mauaji katika ubalozi

Karachi, Pakistan | Machi 8, 1995

Asubuhi ya Machi 8, 1995, gari jeupe ilibeba abiria kwenda kazini kwenye ubalozi mdogo wa Marekani mjini Karachi, Pakistan. Kwenye barabara ya njia panda, teksi ya manjano ilipita mbele ya gari hilo jeupe, na kulilazimisha kusimama wakati gari jingine likiizuia kusogea. Magaidi waliojifunika nyuso zao wakiwa na bunduki za rashasha haraka waliifikia gari hiyo na kufyatua risasi, na kulimiminia risasi na kuvunja madirisha ya gari hilo. Wamarekani wawili wafanyakazi wa ubalozi waliuawa na mmoja alijeruhiwa katika shambulio hilo.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.