Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Jehad Serwan Mostafa

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Jehad Serwan Mostafaanayefahamika kama Ahmed Gurey, Anwar al-Amriki, au Emir Anwar; ni raia wa Marekani na aliyekuwa na makazi katika jimbo la California.  Alishafanya majukumu mbalimbali kwa al-Shabaab ikiwa ni pamoja na mkufunzi wa kambi na kiongozi wa wapiganaji wa ambao ni wageni wa kutoka nchi zingine.  Pia ni mtaalamu wa vyombo vya habari.  Mostafa ni raia wa Marekani ambaye aliishi katika mji wa San Diego, California kabla hajahamia Somalia mnamo mwaka 2005.  Anaweza au kuna uwezekano wa kusafiri katika maeneo haya: Somalia, Yemen, Ethiopia, Kenya na nchi zingine za Afrika.

Mostafa ni gaidi namba moja anayetafutwa na FBI katika orodha ya magaidi watafutwao kwa hali na mali kutokana na matendo yake ya kigaidi.  Mnamo Oktoba 9, 2009 hati ya mahakama ya kukamatwa ilitolewa dhidi ya Mostafa katika mahakama Kuu ya Marekani kupitia Mahakama ya wilaya ya kusini ya California.  Mostafa alishitakiwa kwa makosa yafuatayo: Kula njama kusaidia vifaa/malighafi kwa magaidi, njama kutoa msaada kwa magaidi wan je; na kutoa msaada wa mali kwa makundi ya kigaidi ya nje.

Al-Shabaab ilikuwa ni kikosi cha Kijeshi cha Mahakama ya Kiislamu ya Somalia ambayo ilijitwalia sehemu kubwa ya Kusini mwa Somalia ndani ya nusu ya pili ya mwaka 2006. Al-Shabaab imeendelea na vurugu zake za uasi Somalia-Kusini na Somalia-Kati. Kikundi kimedai kuhusika na milipuko kadhaa, ikiwa ni pamoja na aina mbalimbali za mauaji ya kujitoa mhanga huko Mogadishu na Somalia Kati na Kaskazini, ikilenga hasahasa maafisa wa Serikali ya Somalia na wanaosemekana kuwa Wafuasi wa Serikali ya Mpito ya Muungano (TFG) ya Somalia. Al-shabaab inawezekana ilihusika na wimbi la mfululizo wa milipuko mitano ya kujitoa mhanga kwenye magari mwezi Oktoba, 2008, ambayo kwa wakati mmoja ilipiga maeneo yaliyolengwa kwenye miji miwili Kaskazini mwa Somalia, na kuua watu wasiopungua 26 na kuwajeruhi wengine 29. Al-Shabaab iilihusika na ulipuaji pacha wa jijini Kampala, Uganda, mnamo Julai 11, 2010, ambao uliua zaidi ya watu 70, akiwemo Mmarekani mmoja. Kikundi kinahusika kwa mauaji ya Wahamasishaji wa amani wa Somalia, Wafanyakazi wa Shirika la Misaada la Kimataifa, viongozi kadhaa wa vikundi visivyo vya kiserikali, na waandishi wa habari. Mnamo Februari 2012, al-Shabaab na al-Qaida walitangaza rasmi kushirikiana kwao (kuungana kwao).

Wizara ya Mambo ya Nchi ya Marekani ilikitaja kikundi cha al-Shabaab kuwa kikosi cha Kigaidi cha Uangamizaji wa Wageni, chini ya Kifungu cha Sheria namba 219 cha Uhamiaji na Utaifa (kama kilivyopitishwa) Februari 26, 2008 na ni Kikosi Maalumu cha Ugaidi wa Dunia chini ya Tamko Rasmi Namba 13224, mnamo Februari 29, 2008.

Picha zaidi za

Jehad Serwan Mostafa
Jehad Serwan Mostafa