Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Husayn Muhammed al-Umari

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeidhinisha zawadi ya dola zifikiazo milioni $5 kwa habari zitakazopelekea kukamatwa na/au kufikishwa hatiani kwa Husayn Muhammed al-Umari.

Husayn Mohammed al-Umari anatafutwa na FBI kwa tuhuma za kushiriki kwake katika shambulizi la bomu la Agosti 11, 1982 katika ndege ya Pan American World namba 830, ambalo lilisababisha kuuawa kwa abiria mmoja, kujeruhiwa kwa abiria 16, na jaribio la mauaji ya abiria 267 na wafanyakazi wa ndege katika ndege hiyo. Al-Umari alikuwa mmoja kati ya watu watatu waliofunguliwa mashtaka ya kitendo cha ugaidi na anatuhumiwa kupanga na kutengeneza bomu lililolipuka wakati ndege hiyo ilikuwa hewani kutoka Narita, Japan kuelekea Honolulu, Hawaii.

Al-Umari alifunguliwa mashtaka katika makahama ya District of Columbia kwa: (1) Njama za kufanya mashambulizi na uharibifu wa mali; (2) njama za kufanya mauaji, (3) mauaji; (4) hujuma kwenye ndege; (5) kuharibu ndege inayotumiwa katika biashara ya kigeni (6) kuweka bomu kwenye ndege; (7) ushambuliaji; (8) jaribio la kuhujumu ndege, na (9) kusaidia na kuwezesha. Mwaka 1998, mfanya njama mshiriki, Mohammed Rashed, ambaye alitega bomu kwenye ndege, alikamatwa na kuletwa Marekani. Alikiri kuwa na hatia katika jukumu lake la ushambuliaji wa bomu na kusaini hati ya ushirikiano kama sehemu ya kukiri kwake.

Akiaminika kuwa gwiji hodari wa utengenezaji mabomu na kiongozi wakati mmoja wa kundi la kigaidi la “Mei 15”, al-Umari pia amefunguliwa mashtaka na serikali ya Ufaransa kwa jukumu lake katika shambulizi la bomu mwaka 1985 katika duka la Marks and Spencer mjini Paris na Benki ya Leumi.

Al-Umari huenda anayo hati ya kusafiria ya Lebanon, ambako mke wake inasemekana anaishi. Ni baba wa watoto wawili wa kiume na binti wawili. Aliishi kwa miaka kadhaa nchini Iraq. Ingawa kwa sasa hivi hajulikani alipo, kuna uwezekano anaishi Lebanon au Iraq. Inasemekana kuwa husafiri wakati wote akiwa na silaha na anapaswa kufikiriwa kuwa mwenye silaha na wa hatari.

Picha zaidi za

Husayn Muhammed al-Umari