Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Hasan Izz-al-Din

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Gaidi aliyetajwa hapo juu inaaminika ni mwanachama wa kundi la kigaidi la Lebanon, Hizballah. 

Juni 14, 1985, magaidi waliiteka ndege ya TWA 847 iliyokuwa inatokea Athens, Ugiriki kwenda Roma,Italia. Baada ya kusafiri sehemu kadhaa, ndege hiyo ilitua Beirut, Lebanon, ambako wateka nyara walimpiga risasi na kumuua mzamiaji wa jeshi la majini la Marekani, Robert Stethem na kuutupa mwili kwenye njia ya ndege.

Gaidi aliyetajwa hapo juu alishtakiwa kwa jukumu lake la kupanga na kushiriki katika utekaji nyara wa ndege ya biashara Juni 14, 1985. Utekaji nyara ulisababisha mashambulizi kwa abiria kadhaa na wafanyakazi wa ndani ya ndege na mauaji ya raia mmoja wa Marekani.

Mtu aliyetajwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Njama za kutenda uharamia katika ndege, kuwakamata mateka, na kutenda uharamia wa angani uliosababisha mauaji, kuingilia kati wafanyakazi wa ndani ya ndege, kuweka vitu vya uharibifu ndani ya ndege, kuwa na milipuko ndani ya ndege, na kushambulia abiria na wafanyakazi; uharamia wa angani uliosababisha mauaji; uharamia wa angani; kufanya utekaji; kuingilia kati wafanyakazi; kuweka milipuko ndani ya ndege; kuweka vifaa vya uharibifu ndani ya ndege; kufanya mashambulzi ndani ya ndege kwa nia ya kufanya utekaji kwa kutumia silaha za hatari na kusabaisha madhara ya kimwili; na kutoa msaada na kushiriki.