Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Hamad el Khairy

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Hamad el Khairy ni kiongozi na mwanachama mwanzilishi wa kundi la kigaidi la Harakati za Umoja na Jihadi Afrika Magharibi (MUJWA, Pia linafahamika kama MUJAO na TWJWA). Chini ya uongozi wa Khairy, wanachama wa MUJWA wamefanya operesheni za utekaji nyara, mashambulizi ya kigaidi na utekaji nyara wa wanadiplomasia. Khairy alijitangaza kuhusika kwenye utekaji nyara wa Aprili 2012 wa wanadiplomasia saba wa Algeria huko Mali, na ameonekana katika video za MUJWA akitoa vitisho dhidi ya wale wanaopinga chama chao. Mnamo Januari 2012, Khairy alitamka kwamba lengo la MUJWA lilikua “kuanzisha utawala wa sharia maeneo yote ya Afrika Magharibi”.

Kabla ya uongozi wake ndani ya MUJWA, Khairy alikuwa mwanachama wa AQIM, uandaaji mipango ya kigaidi dhidi ya Mauritania. Mnamo Oktoba 2011, Khairy alitoa amri ya utekwaji wa wafanyakazi watatu wa shirika la utoaji misaada toka Ulaya huko Algeria, na kuacha wawili wamejeruhiwa na risasi. Khairy alitangazwa rasmi kuwa gaidi kwa hati maalum 13224 mnamo Desemba 7, 2012.

MUJWA ilianzishwa mnamo Septemba 2011 kama kundi la pembeni la al-Qaida ndani ya Ardhi ya Kiislam Maghreb (AQIM) ili kueneza shughuli za kigaidi kote Afrika Magharibi. MUJWA imefanya mashambulizi mbalimbali na utekaji, ukijumlisha na shambulio la Machi 2012 huko Tamanrasset, Algeria, ambapo watu 23 walijeruhiwa. MUJWA pia ilitangaza kuhusika na utekwaji wa Balozi wa Canada na mjumbe wa Umoja wa Mataifa Robert Fowler. Marekani ilitangaza MUJWA kuwa kundi hatari la kigaidi mnamo Desemba 7, 2012, na Kamati ya Vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya al-Qaida iliitaja MUJWA mnamo Desemba 5, 2012, kwa ushirikiano na AQIM.