Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Hafiz Saeed

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 10

Hafiz Mohammad Saeed ni profesa mstaafu wa Kiarabu na Uhandisi, na vilevile ni mwanachama mwanzilishi wa Jamaat-ud-Dawa, chama cha Kiislamu cha Ahl-e-Hadith chenye msimamo mkali kinachojishulilisha na kuweka kanuni za Kiislamu sehemu za India na Pakistani, na tawi lake la Kijeshi, Lashkar-e-Tayyiba. Saidi (saeed) anatuhumiwa kwa kuratibu vamizi kadhaa za kigaidi, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa mwaka 2008, Mumbai ambao ulipelekea vifo vya watu 166, wakiwemo raia sita wa Marekani.

Serikali ya India imetoa tangazo kupitia Polisi wa Kimataifa dhidi ya Saeed kwa uhusika wake kwenye uvamizi wa kigaidi wa Mumbai, mwaka 2008. Kwa nyongeza, Wizara ya Fedha ya Marekani imemtaja Saeed kama mlengwa Kitaifa chini ya Kifungo namba 13224. Saeed pia alitajwa binafsi na Umoja wa Mataifa chini ya Kifungu cha UNSCR 1267, Desemba 2008.

Lashkar-e-Tayyiba ilitajwa kama kikundi cha Kigeni cha Kigaidi mnamo Desemba 2001. Mnamo Aprili 2008, Marekani ilitaja Jamaat-ud-Dawa kama kikundi cha Kigeni cha Ugaidi; sambamba na hilo, Umoja wa Mataifa ulikitangaza “Jamaat-ud-Dawa” kuwa kikundi cha Kigaidi Dedemba 2008.