Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Hafiz Abdul Rahman Makki

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 2

Hafiz Abdul Rahman Makki ni naibu kamanda wa Lashkar-e-Tayyiba, kikundi cha Kiislamu cha Ahl-e-Hadith chenye msimamo mkali, ambacho kinajishughulisha na kusambaza kanuni za Kiislamu nchini India na Pakistani. Lashkar-e-Tayyib inasadikika kupanga na kutekeleza uvamizi wa kigaidi mnamo Novemba 2008, huko Mumbai, ambao ulisababisha vifo vya watu 166 wakiwemo raia sita wa Kimarekani, ikiwa ni pamoja na matukio mengine ya ugaidi nchini India.

Wizara ya Fedha ya Marekani imemtangaza Makki kama Mteule Kitaifa chini ya Sheria namba 13224.

Lashkar-e-Tayyiba alitangazwa kama kikundi cha Ugaidi cha Kigeni mnamo Desemba 2001. Mnamo Aprili 2008, serikali ya Marekaniilitangaza Jamaat-ud-Dawa kuwa kikundi cha Kigeni cha Ugaidi; vilevile, Serikali ya Marekani ilikitangaza Jamaat-ud-Dawa kama kikundi cha Ugaidi mnao Desemba 2008.