Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Gulmurod Khalimov

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Aliyekuwa kanali wa kikosi cha ukomandoo cha Tajikistan, kamanda wa polisi, na snaipa wa jeshi Gulmurod Khalimov ni mwanachama wa Dola ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) na mshawishi wa wanachama wapya kujiunga. Yeye alikuwa ni kamanda wa wa kikosi maalumu cha kijeshi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tajikistan. Khalimov aliotokea kwenye video ya kipropaganda kuthibitisha kwamba anapigana tokea ISIL na akatoa wito wa wazi wa vitendo vya kihalifu dhidi ya Wamarekani.

Mnamo Septemba 29, 2015, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alimtambulisha Khalimov kama Gaidi la Kimataifa chini ya Hati ya Kiutendaji 13224. Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa 1267/1989/2253 ISIL (Da’esh) na Kamati ya Vikwazo ya al-Qaida ilimuongeza kwenye orodha ya wenye vikwazo mnamo Februari 2016. Khalimov anatafutwa na Serikali ya Tajikistan.

Picha zaidi za

Gulmurod Khalimov
Gulmurod Khalimov
Gulmurod Khalimov
Gulmurod Khalimov
Gulmurod Khalimov - English