Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Kupigwa bomu kwa msafara wa kidiplomasia wa Marekani

Beit Hanoun, Ukanda wa Gaza | Oktoba 15, 2003

Oktoba 15, 2003, Wamarekani watatu waliuawa na mmoja kujeruhiwa vibaya na bomu la kando ya barabarani huko Beit Hanoun, Ukanda wa Gaza. Waathirika walikuwa wakitoa ulinzi kwa wawakilishi kutoka ofisi ya Mjumbe wa Marekani kwa Mashariki ya kati, wakati akielekea Gaza kwa mahojiano na Wapalestina waliokuwa wameomba kujiunga na mpango wa masomo wa Fulbright.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.