Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Faker Ben Abdelaziz Boussora

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Fakeri Boussora, pia anajulikana kama Abu Yusif al-Tunisi, ni raia wa Tunisia mwenye uhusiano mkubwa na waislamu wenye msimamo mkali. Yeye alipatiwa mafunzo na al-Qaida na alitangaza azma ya kujitoa mhanga. Boussora ni mshirika wa mshukiwa wa ugaidi na raia wa Tunisia Abderraouf Jdey, na watu hao wawili huenda walisafiri pamoja siku zilizopita.

Boussora aiondoka nchini kwake Tunisia mwaka 1988 na kuhamia Ufaransa. Aliondoka Ufaransa mwaka 1991, na kuhamia Montreal, Canada, alisafiri kwenda na kurudi kutoka Canada na Tunisia mara kwa mara katika miaka ya 1990. Boussora alipata uraia wa Canada mwaka 1999 na wakati akiwa Canada alihudhuria Msikiti wa Assuna huko Montreal.

Boussora aliondoka Canada mwaka 1999 na huenda alifanya zaidi ya safari moja kwenda Afghanistan katika kipindi cha miaka ya 1999 – 2000. Alipata mafunzo kutoka al-Qaida wakati akiwa nchini Afghanistan, na mara kwa mara alirejea Canada.

Mamlaka zinaendelea kuwa na wasi wasi kwamba Boussoura huenda akajaribu kurejea Canada au Marekani kupanga au kushiriki katika shambulizi la kigaidi. Huenda anaathiriwa na maradhi makubwa na huenda afya yake ni mbaya sana, matokeo yakiwa ni kukonda na kubadilika hali yake ya kimwili.