Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Kushambuliwa kwa watalii

Hifadhi ya Bwindi, Uganda | Machi 1, 1999

Machi 1, 1999, kundi la wanajeshi 100 wa Interahamwe walishambulia watalii wasiokuwa na silaha na walinzi wao katika hifadhi ya taifa ya Bwindi nchini Uganda. Interahamwe ni kundi la wanamgambo lililoundwa na kundi la vijana wa Kihutu ambao walifanya vitendo vya mauaji ya halaiki nchini Rwanda dhidi ya Watusi mwaka 1994.

Katika shambulizi la hifadhi ya Bwindi, makundi kadhaa ya kitalii yalishambuliwa, kuchukuliwa mateka na kulazimishwa kutembea kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mganda mmoja, Paul Ross Wagaba, alichomwa moto akiwa hai. Wahanga wanane, wakiwemo Wamarekani Susan Miller na Robert Haubner, walipigwa hadi kufa.

Vitu vingi viliibiwa kutoka kwa watalii wakati wa shambulizi, ikiwemo hati ya kusafiria ya Marekani, Leseni ya gari iliyotolewa Marekani, Saa ya kike aina ya Citizen na kompyuta – laptop, aina ya Toshiba Portogo.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.