Tendo la Kigaidi
Maelezo juu ya…

Shambulio la kigaidi dhidi ya eneo maalum la Kimarekani na eneo la nyongeza huko Benghazi, Libya

Benghazi, Libya|Septemba 11-12, 2012

Mnamo Septemba 11-12, 2012, Wamarekani wanne – Balozi wa Marekani nchini Libya John Christopher Stevens, Ofisa wa Habari, Usimamizi na Huduma za Nje Sean Smith, na Mtaalam wa Usalama Glen Anthony Doherty na Tyrone Snowden Woods – waliuawa katika shambulio la kigaidi dhidi ya eneo maalum la Kimarekani na eneo la nyongeza huko Benghazi, Libya. Mfululizo wa mashambulizi ikijumuisha uchomaji, bunduki na maguruneti yanayoongozwa na makombora (RPGs) na vinu yalielekezwa katika vituo viwili vya Marekani huko Benghazi, pamoja na wafanyakazi waliopo katika vituo hivyo viwili. Aidha, mashambulizi yaliwajeruhi vibaya sana wanafanyakazi wawili wa Kimarekani, kuwajeruhi walinzi watatu wa mkataba wa Libya, na kusababisha uharibifu na kutelekezwa kwa vituo hivyo viwili.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni 10 kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.

Balozi John Christopher Stevens, umri miaka 52, alizaliwa Kaskazini mwa California na alianza kazi katika Huduma ya Mambo ya Nje mnamo mwaka 1991. Balozi Stevens alifanya kazi nyingi majukumu nje ya nchi na alikuwa Naibu Mkuu wa Misheni nchini Libya kuanzia mwaka 2007 hadi 2009. Kuanzia Machi 2011 hadi Novemba 2011, Balozi Stevens alifanya kazi kama Mjumbe Maalum kwa Baraza la Mpito la Taifa la Libya, na aliwasili mjini Tripoli mnamo Mei 2012 kama Balozi wa Marekani nchini Libya. Kabla ya kuingia katika Huduma za Mambo ya Nje, Balozi Stevens alikuwa mwanasheria wa mambo ya biashara za kimataifa huko Washington, DC, na kabla ya hapo alifundisha Kiingereza kwa kujitolea kupitia Peace Corps nchini Morocco kuanzia 1983 hadi 1985. Waziri wa mambo ya Nje Hillary Rodham Clinton alimtambua Balozi Stevens kama “Shujaa na mtu mwema, mwanadiplomasia aliyebobea na shujaa wa Marekani”.

Sean Smith, miaka 34, alizaliwa San Diego, California, na alijiunga na Jeshi la Anga la Marekani mnamo mwaka 1995 kama Mtaalam wa kutengeneza redio na Stafu Sajenti. Smith alijiunga na Huduma za Mambo ya Nje mnamo mwaka 2002 kama Ofisa wa Habari na Usimamizi, kufanya kazi katika majukumu mbalimbali nje ya nchi, kujumuisha Baghdad, Petrolia, Motreal, na Hague. Smith alisafiri kwenda Benghazi, Libya mnamo Septemba 2012 kwa ajili ya kutoa msaada wa mawasiliano na usimamizi kwa Misheni Maalum ya Marekani.

Glen Anthony Doherty, miaka 42, alizaliwa Winchester, Massachusetts, na alijiunga Jeshi la Maji la Marekani kama Komandoo (Navy SEAL) mnamo mwaka 1995, na kufanya kazi huko Iraq na Afghanistan katika kipindi cha uanajeshi wake. Kabla ya kujiunga na Jeshi la Maji, Doherty pia alifanya kazi kama mwalimu mtaalam wa Ski, alihudhuria shule ya urubani, na alikuwa mtaalam aliyebobea kwenye huduma ya kwanza na mkufunzi wa urubani. Mnamo mwaka 2005 Doherty alianza kufanya kazi kwenye kampuni binfasi inayotoa huduma za usalama kwa wafanyakazi wa Kimarekani nje ya nchi. Doherty alisafiri kwenda Benghazi, Libya mnamo Septemba 2012 kwa ajili ya kutoa huduma ya usalama kwa Misheni Maalum ya Marekani.

Tyrone Snowden Woods, miaka 41, alizaliwa mjini Portland, Oregon, na alifanya kazi kwa miaka ishirini kama Komandoo wa Jeshi la Maji la Marekani (Navy SEAL), kufanya kazi katika operesheni mbalimbali huko Somalia, Iraq na Afghanistan. Woods pia alikuwa ni Nesi aliyesajiliwa na mtaalam aliyethibitishwa kwa huduma ya kwanza. Mnamo mwaka 2010, Woods alianza kutoa huduma ya usalama kwa wafanyakazi wa kimarekani nje ya nchi kupitia kampuni binafsi iliyopewa mkataba. Woods alisafiri kwenda Benghazi, Libya mnamo Septemba 2012 kwa ajili ya kutoa huduma ya usalama kwa Misheni Maalum ya Marekani.

Waathirika

Picha ya John Christopher Stevens
John Christopher Stevens
Picha ya Sean Smith
Sean Smith
Picha ya Glen Anthony Doherty
Glen Anthony Doherty
Picha ya Tyrone Snowden Woods
Tyrone Snowden Woods