Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Amir Muhammad Sa’id Abdal-Rahman al-Mawla

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Al-Mawla, anayejulikana pia kama Hajji ‘Abdallah, ni kiongozi wa juu wa Jimbo la Iraqi na Syria (ISIS). Alikuwa msomi wa kidini katika shirika la utangulizi la ISIS, al-Qaida huko Iraqi (AQI), kwa udhabiti alipanda cheo na kuchukua jukumu la uongozi wa juu wa ISIS.

Kama mmoja wa mtaalam mkuu wa itikadi kali zaidi za ISIS, Hajji ‘Abdallah alisaidia kuendesha na kuhalalisha kutekwa, kuchinjwa, na usafirishaji wa wachache wa dini ya Yazidi kaskazini magharibi mwa Iraq na inaaminika alisimamia shughuli kadhaa za kigaidi duniani. Yeye anaweza kufanikiwa kuwa mrithi wa kiongozi wa ISIS Abu Bakr al-Baghdadi.

Mnamo Juni 2014, ISIS, pia inajulikana kama Da’esh, ilichukua udhibiti wa sehemu za Syria na Iraqi, ikajitangaza kuwa “ukhalifa” wa Kiislam, na kumtaja al-Baghdadi kama “khalifa.” Katika miaka ya hivi karibuni, ISIS ilipata utii wa vikundi vya jihadist na watu waliokua ulimwenguni kote, na kuhamasisha mashambulizi kote ulimwenguni.

Zawadi hii ni wakati muhimu katika vita yetu dhidi ya ISIS. Kama ISIS imeshindwa kwenye uwanja wa vita, tumeazimia kutambua na kupataviongozi wa kikundi ili muungano wa kimataifa wa mataifa yanayopigania kuishinda ISIS unaweza kuendelea kuharibu mabaki ya ISIS na kuzuia matarajio yake ya ulimwengu.

Picha zaidi za

Amir Muhammad Sa’id Abdal-Rahman al-Mawla