Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Ali Sayyid Muhamed Mustafa al-Bakri

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Ali Sayyid Muhamed Mustafa al-Bakri ni mwanachama wa al-Qa’ida na mjuzi wa kulipua mabomu na silaha za kemikali. Yeye ni mwanachama wa al-Qa’ida wa baraza la Shura na ana ushirikiano wa karibu wa wakubwa wa al-Qa’ida Saif al-Adel na Ayman al-Zawahiri.

Kabla ya kujiunga na al-Qa’ida, al-Bakri alikuwa mwanachama wa Egyptian Islamic Jihad, kundi la kigaidi chini ya uongozi wa al-Zawahiri. Alikuwa mwalimu katika kambi ya al-Qa’ida huko Afghanistan, akitoa mafunzo ya kutumia milipuko na silaha za kemikali kwa magaidi wapya. Al-Bakri pia alijaribu kuteka ndege ya abiria ya Pakistani Desemba mwaka 2000 lakini hakufanikiwa. Inaelekea bado anaendelea kutoa mafunzo kwa magaidi wa al-Qa’ida na watu wengine wenye msimamo mkali.