Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Ahlam Ahmad al-Tamimi

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Raia wa Jordan, Ahlam Ahmad al-Tamimi, pia anajulikana kama “Khalti” na “Halati,” ni gaidi mwendeshaji wa HAMAS aliyehukumiwa.

Mnamo Agosti 9, 2001, al-Tamimi alisafirisha bomu na mtoa mhanga wa bomu wa HAMAS kwenda Yerusalemu Sbarro pizzeria iliyojaa watu wengi, ambako mshambuliaji alilipua mabomu, na kuua watu 15, ikiwa ni pamoja na watoto saba. Raia wawili wa Marekani waliuawa katika shambulio – Judith Shoshana Greenbaum, mwalimu mjamzito mwenye umri wa miaka 31 kutoka New Jersey, na Malka Chana Roth, mwenye umri wa miaka 15. Wengine zaidi ya 120 walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na Wamarekani wanne. HAMAS walidai kuhusika na mabomu.

Mwaka 2003, al-Tamimi alikiri kosa kwenye mahakama ya Israel la kushiriki katika shambulio hilo na alihukumiwa vifungo 16 vya maisha nchini Israeli kwa kumsaidia mshambuliaji. Alitolewa mnamo Oktoba 2011 kama sehemu ya kubadilishana wafungwa kati ya Hamas na Israeli. Mnamo Machi 14, 2017, U.S. Idara ya Haki ilifungua malalamiko ya makosa ya jinai na hati ya kukamatwa kwa al-Tamimi, kumshtaki chini ya sheria ya Marekani kwa “kula njama kutumia silaha ya uharibifu mkubwa dhidi ya raia wa Marekani nje ya Marekani, na kusababisha kifo.” FBI pia ilimuongeza al-Tamimi kwenye orodha yake ya magaidi wanaotafutwa sana na kumfikiria/kumuona kama mwenye “silaha na hatari.”

Mwanafunzi wa zamani akifanya kazi kama sehemu ya masaa kama mwandishi wa televisheni, al-Tamimi alimuendesha mshambuliaji kwenye lengo baada ya kuahidi kutekeleza mashambulizi kwa niaba ya mrengo wa kijeshi wa HAMAS, kulingana na FBI. Al-Tamimi, ambaye alipanga na kuunda shambulio la Sbarro, alichagua eneo hilo kwa sababu ilikuwa mgahawa ulio na shughuli nyingi. Ili kupunguza tuhuma, yeye na mshambuliaji wa kujitoa mhanga walivaa kama Waisraeli, na yeye mwenyewe alisafirisha/beba bomu, alificha ndani ya kesi/begi la gitaa, kutoka mji wa Magharibi hadi Yerusalemu. Al-Tamimi pia alikiri kulipua bomu dogo kwenye duka ndani ya Yerusalemu wiki chache kabla ya shambulio kama jaribio.

Hamas imechaguliwa na Idara ya Nchi kama Shirika la Ugaidi wa Mambo ya Nje (FTO) chini ya Sheria ya Uhamiaji na Raia na kama Shirika la Kimataifa la Ugaidi (SDGT) chini ya E.O. 13224.

Zawadi kwa ajili ya Programu ya Haki inatoa/inaofa hadi dola millioni 5 kwa habari itakayopelekea kukamatwa kwa al-Tamimi au kuhukumiwa kwa kuhusika kwake katika shambulio hili, kama sehemu ya unyanyasaji wa mwaka 1993 katika upinzani dhidi ya majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati.

Picha za ziada

Malka Chana Roth
Malka Chana Roth
Judith Shoshana Greenbaum
Judith Shoshana Greenbaum
Shambulio la Mabomu Sbarro Pizzeria mwaka 2001
Shambulio la Mabomu Sbarro Pizzeria mwaka 2001
Ahlam Ahmad al-Tamimi
Ahlam Ahmad al-Tamimi