Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abubakar Shekau

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 7

Abubakar Shekau ni kiongozi wa Jama’atu Ahl as-Sunnah il-Da’awati linalofahamika zaidi kama Boko Haram.  Boko Hara mina maana “Elimu ya Magharibi hairuhusiwi” ni kikundi cha kigaidi kilichojikita nchini Nigeria kinachotaka kuipindua serikali ya sasa ya Nigeria na kuanzisha utawala wa sheria za Kiislamu.  Kikundi hiki kimekuwepo katika mifumo tofauti tangu mwishoni mwa miaka ya 1990. Kuna taarifa za mawasiliano, mafunzo na silaha zinazowahusisha kati ya Boko Haram, al-Qaida katika Ardhi ya Kiislamu ya Maghreb (AQIM), al-Shabaab, na al-Qaida katika Penisula ya Uarabuni, kitu ambacho kinaweza kuimarisha uwezo wa Boko Haram kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Awali, Shekau alikuwa mkuu wa pili kimadaraka katika kikundi. Mnamo Julai 2010, Shekau bila kujificha alijitangaza kuchukua uongozi wa juu wa Boko Haram na kutishia kufanya mashambulizi katika sehemu zenye maslahi ya Magharibi nchini Nigeria.  Mbeleni katika mwezi huo, Shekau alitoa tamko la pili kelezea ushirikiano imara walionao na al-Qaida na kuitisha Marekani. Chini ya utawala wa Shekau, uwezo wa Boko Haram umezidi kukua.

Kikundi hiki kiliweza kutengeneza kifaa chao cha kwanza cha mlipuko wa motokaa (IED) mnamo Juni 2011, na kimezidi kutumia IED katika sehemu zenye maslahi madogo.  Shambulio la Boko Haram la mnamo Agosti 26, 2011 la mlipuko wa bomu kwenye motokaa katika makao makuu ya Umoja wa Matifa mjini Abuja, Nigeria yalitambuliwa kuwa shambulio la kwanza ziton la kikundi hicho dhidi ya maslahi ya Magharibi.  Walau watu 23 waliuawa, na zaidi ya 80 walijeruhiwa katika mlipuko huo. Msemaji wa Boko Haram alitamba na kutangaza uhusika wa kikundi chao katika mlipuko huo na kuahidi mashambulio mengine dhidi ya Marekani na maslahi ya serikali ya Nigeria.

Mnamo Mei 1, 2012 chini ya kipindi cha wiki moja baada ya kikundi hicho kulipua jingo la magazeti ya Nigeria mjini Abuja, Boko Haram walitoa tamko kupitia mkanda wa video kutishia mashambulizi zaidi dhidi ya vyombo vya habari vya ndani na kimataifa, ikiwamo Sauti ya Amerika na Waandishi wa Sahara, chombo cha habari chenye makao huko New York.

Chini ya uongozi wa Shekau, Boko Haram imeendelea kuwalenga watoto wadogo. Mnamo Aprili 14, 2014, Boko Haram iliwateka nyara karibia wasichana 300 kutoka katika shule yao huko kaskazini mwa Nigeria. Katika ujumbe wa video uliotolewa wiki tatu zilizoppita, Shekau ilitamba kuhusika na utekaji nyara, kuwaita wasichana watumwa na kuwatishia kuwauza katika soko.

Mnamo Juni 21, 2012, Wizara ya Mambo ya Ndani ilimtambulisha rasmi Shekau kama Gaidi wa Kimataifa chini ya Waraka Maalum 13224.