Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abu Ubaidah (Direye)

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 6

Abu Ubaidah (Direye) ni kiongozi wa al-Shabaab. Msemaji wa al-Shabaab, Ahmed Abdi aw Mohamed, alimtangaza Abu Ubaidah kama kiongozi wa kundi mnamo Septemba 6, 2014, baada ya kifo cha kiongozi wa awali wa al-shabaab amir Ahmed Abdi aw-Mohamed (Godane). Abu Ubaidah alikuwa mmoja wa watu wa ndani muhimu wakati wa kifo cha Godane. Umoja wa Mataifa ulimuweka katika vikwazo kwa mujibu wa aya ya 8 ya Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 1844 mnamo Septemba 24, 2014.

Anasadikika kuwa mfuasi wa mtazamo wa Godane kwamba al-Shabaab ni zaidi ya harakati za kizalendo za Somalia bali ni moja mstari wa mbele katika harakati za jihadi za al-Qaida ulimwenguni.

Kama amir, Abu Ubaidah ni mhusika wa moja kwa moja kwa shughuli za al-shabaab, ambazo zinazidi kuhatarisha amani, usalama na uimara wa Somalia na maslahi ya Marekani katika eneo. Anasadikiwa kuwa katika miaka yake ya arobaini na mtu koo ya Dir kutoka mkoa wa Kismayo nchini Somalia.