Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abu-Muhammad al-Shimali

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Mwandamizi wa juu wa serikali ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) Mkuu wa mpaka Tirad al-Jarba, anayejulikana zaidi kama Abu-Muhammad al-Shimali, amekua akijihusisha na ISIL, zamani ikijulikana kama al-Qaeda nchini Iraq, tangu mwaka 2005. Sasa anatumika kama ofisa muhimu katika kamati ya Uhamiaji na Vifaa (usafirishaji), na anahusika na ufanikishaji wa usafiri wa wapiganaji wa kigeni wa kigaidi hasa kwa kupitia Gaziantep, Uturuki, na kuendelea mpaka kwenye mji ulio mpakani wa Jarabulus nchini Syria, unaodhibitiwa na ISIL. Al-Shimali na kamati ya Uhamiaji na Vifaa (usafirishaji) wanaratibu shughuli za magendo, uhamisho wa fedha, na harakati za uhamishaji/usafirishaji wa vifaa ndani ya Syria na Iraq kutoka Ulaya, Afrika Kaskazini, na Peninsula ya Arabia. Mnamo mwaka2014, al-Shimali alifanikisha/aliwezesha usafiri wa wapiginaji wa ISIL kutoka Uturuki hadi Syria kwa wapiganaji kutoka Australia, Ulaya, na Mashariki ya Kati, na kusimamia kituo cha kusindika/kushughulikia askari wapya ndani ya Azazi, Syria.

Marekani na Muungano wa Kimataifa wa mashirika zaidi ya 60 ya kimataifa wana jukumu la kuidhalilisha, na hatimaye kuishinda, ISIL.Ili Kufikia lengo hili juhudi nyingi zinahitajika , pande zote kuimarisha mistari ya juhudi.Moja ya juhudi muhimu za umoja ni kuzuia mtiririko wa wapiganaji wa kigaidi wa kigeni. Mbinu hii inaleta usalama wa nchi wa pamoja, utekelezaji wa sheria, sekta ya haki, akili, diplomasia, jeshi, uwezo wa kujenga, na juhudi za kubadilishana taarifa.

Zaidi ya wapiganaji wa kigaidi wa kigeni 25,000 kutoka nchi zaidi ya 100 wamesafiri kwenda Iraq na Syria. Mapigano ndani ya Iraq na Syria yanawapa wapiganaji wa kigeni wa kigaidi uzoefu wa vita , silaha na mafunzo ya mabomu/milipuko, na upatikanaji wa mitandao ya kigaidi ambayo inaweza kuwa inapanga mashambulizi ambayo yanalenga nchi za Magharibi. Tishio la Pamoja la mpiganaji wa kigaidi wa kigeni limekuza ushirikiano wa karibu miongoni mwa vyombo vya serikali ya Marekani na Mashirika ya kimataifa, ambao watatumia njia zote zilizopo kuvuruga mtiririko wa wapiganaji na hatimaye kuishinda ISIL.