Silaha za Maangamizi

Magaidi wenye azma ya kupata na kuzitumia silaha za maangamizi (WMD) ni tishio kubwa kwa amani ya kimataifa na ulinzi. WMD zinaweza kuua idadi kubwa ya raia na kuvizidi nguvu vikosi vya kutoa msaada wa dharura.Silaha za maangamizi ni pamoja na silaha za nyuklia, kemikali, kibailojia na za mionzi, pamoja na mabomu yenye uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa.

Marekani ina nia ya dhati kuwazuia magaidi wasitumie silaha hizi zenye uharibifu mkubwa.

Kama utatoa habari ambayo itapelekea kukamatwa au kushtakiwa kwa mtu yoyote anayetenda, anayejaribu au kula njama za kutenda au kusaidia na kushiriki katika kitendo cha ugaidi wa kimataifa kinachohusisha silaha za maangamizi dhidi ya Wamarekani au mali za Marekani popote duniani, huenda ukastahili kupewa tuzo.

Muhimu: Dai lolote la uongo wa makusudi litaripotiwa kwa mamlaka husika.

Mnamo Julai15, 2006, Rais Bush na Rais Putin walizindua juhudi za ulimwengu za kupambana na ugaidi wa silaha za nyuklia. Lengo la juhudi hii ya kipekee ni kupanua na kuimarisha ushirikiano katika kupambana na tishio la ugaidi wa nyuklia.