Habari za ushuhuda wa Mafanikio

Mpango wa zawadi nono za Haki umelipa zaidi ya dola milioni 150 kwa watu zaidi ya 100 ambao walitoa taarifa iliyozuia mashambulizi ya magaidi wa kimataifa au imesaidia kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na vitendo vya awali.

Watu wenye ujasiri na wenye nia ya kujitokeza wakiwa na taarifa ambazo pia zimesaidia kuzuia na kutatua mashambulizi ya kigaidi:

  • RFJ ilifanya malipo ya mamilioni ya dola mwaka 2019 ambayo ilileta haki kwa kiongozi mkuu wa ISIS katika Mashariki ya Kati.
  • Wakati wa vita vya Ghuba, mtoa taarifa ambaye ni jasiri kutoka nchi ya Mashariki mwa Asia alijitokeza mbele na habari za kushtusha kuhusu mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi yaliyopangwa. Magaidi walikuwa tayari wamekagua maeneo waliyokusudia na waliweka pamoja silaha zenye kujiendesha zenyewe moja kwa moja, magruneti na milipuko. Masaa 48 tu kabla ya shambulizi la kwanza kati ya mashambulizi yaliyopangwa, mtoa habari alifichua habari muhimu ambazo zilizuia mpango wa magaidi. Shambulizi lilisimamishwa, kijana alipewa zawadi nono, na familia yake ilihamishiwa sehemu salama. Kwa kutoa habari mtu huyu ameokoa maisha ya mamia ya watu.
  • Katika kesi nyingine, msichana alijitokeza na habari kuhusu watu walioiteka ndege na kuwapiga kikatili abiria waliokuwa ndani. Alieleza kuwa”alihisi mwenye nguvu lazima haki itendeke.” Kiongozi wa wateka nyara alirudishwa Marekani na kufungwa kwa mashtaka ya uharamia wa ndege. Msichana alipewa zawadi nono kwa jitihada za kupiga vita ugaidi.
  • Msichana mwingine mwanafunzi katika chuo kikuu cha kigeni, alishuhudia mauaji ya kikatili ya mwanadiplomasia wa Marekani. Kutokana na habari alizozitoa, washambuliaji wawili walihukumiwa kifungo cha maisha. Mwanafunzi na familia yake walihamishwa kwenye makao salama na alipokea zawadi nono.