Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

 • Je unaweza kutoa taarifa kuhusu Mpango wa zawadi nono wa Haki (RFJ)?

  Je unaweza kutoa taarifa kuhusu Mpango wa zawadi nono wa Haki (RFJ)?

  • Programu ya zawadi ya Idara ya Taifa ya Marekani ya Kupambana na Ugaidi, ilianzishwa kwa Sheria ya 1984 ili Kupambana na ugaidi wa kimataifa, sheria ya umma 98-533 (iliyosimbikwa katika 22 U.S.C. § 2708. Ikisimamiwa na Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Usalama wa kidiplomasia, lengo la RFJ ni kuleta magaidi wa kimataifa kwenye haki na kuzuia vitendo vya ugaidi wa kimataifa dhidi ya watu au mali za U.S. Chini ya mpango huu, Katibu wa Jimbo anaweza kuidhinisha tuzo kwa habari ambayo imepelekea kukamatwa au kushtakiwa kwa mtu yeyote ambaye anapanga, anatenda, anasaidia, au anayejaribu vitendo vya kigaidi ya kimataifa dhidi ya watu au mali za Marekani, kwamba kuzuia vitendo hivyo visitokee hapo awali, ambayo itapelekea kutambuliwa au eneo la kiongozi muhimu wa kigaidi, au kwamba itakayosumbua ufadhili wa ugaidi.

   RFJ inatunza orodha ya zawadi nono zinazotolewa kwenye tovuti yake: www.rewardsforjustice.net. Tuzo nyingi za RFJ ni dola zinazofikia milioni tano. Hata hivyo, tuzo zinazotolewa zinaweza kuanzia chini ya dola milioni moja mpaka dola milioni 25. Kwa kuongezea, RFJ inaweza pia kulipa tuzo katika kesi ambazo hakuna tuzo za awali ambazo zimetolewa, katika hali zinazostahili.

   Tangu kuanzishwa kwake, RFJ imelipa zaidi ya dola milioni 150 kwa watu zaidi ya 100 kwa habari ambazo zimepelekea kuzuia mashambulizi ya ugaidi wa kimataifa au kusaidia kuwafikisha wale waliohusika na vitendo hivyo vya awali.

 • RFJ imefanikiwa kiasi gani?

  RFJ imefanikiwa kiasi gani?

  • Kuhusiana na mradi wa RFJ, vyanzo vinaweza kutoa habari ambazo zimesaidia kuzuia au kusuluhisha vitendo vya ugaidi wa kimataifa dhidi ya maslahi ya Marekani na kuwafikisha mbele ya sheria magaidi hatari sana hapa duniani. Juhudi hizi zimesaidia kuokoa maisha ya watu wasiokuwa na hatia.

   Nchini Iraq, kwa mfano, siku 18 tu baada ya kutangazwa kwa zawadi nono kwa ajili ya Uday na Qusay Hussein, chanzo kilijitokeza na kutoa habari kuhusiana na mahali walipo. Mafanikio mengine yaliyotangazwa sana ni kukamatwa kwa Ramzi Yousef, mmoja wa walipuaji mabomu mwaka 1993 kwenye kituo cha biashara cha World Trade Center, ambaye aligundulika mwaka 1995, ikiwa ni matokeo ya habari zilizotolewa na chanzo kwa kuitikia tangazo la zawadi nono lililotolewa na RFJ.

 • Zawadi nono zinazotolewa zinatangazwa vipi?

  Zawadi nono zinazotolewa zinatangazwa vipi?

  • Mbali na tovuti ya RFJ, tunatumia mabango, vijitabu, matangazo ya malipo kwenye radio na kwenye magazeti, mtandao na kwenye sehemu yoyote muafaka kusaidia kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Marekani.

 • Taarifa zipi unazitoa kuhusu malipo ya zawadi nono?

  Taarifa zipi unazitoa kuhusu malipo ya zawadi nono?

  • Kiungo muhimu cha mradi huu ni kwamba tunahakikisha majibu kwa kampeni yetu ya tuzo yanakuwa siri kubwa. Na lililo muhimu zaidi, hatutoi majina ya watu ambao wamelipwa tuzo, na kwa kawaida hatutoi hadharani maelezo yoyote kuhusu tuzo zilizolipwa. Na katika kesi za wahalifu muhimu, tunatangaza malipo ya tuzo, lakini hatutoi habari zaidi.

 • Je unaweza kutoa maelezo bayana kuhusu malipo zawadi nono?

  Je unaweza kutoa maelezo bayana kuhusu malipo zawadi nono?

  • Malipo makubwa yaliyotolewa hadi hivi leo ni dola milioni 30 kwa mtu mmoja ambaye alitoa habari ambazo zilipelekea kukamatwa kwa Uday na Qusay Hussein.

   Kumekuwepo sherehe nne za tuzo za RFJ huko Phillipines. Tuzo ya karibuni ilikuwa June 7, 2007, na jumla ya tuzo iliyotolewa katika sherehe hiyo ilifikia dola milioni 10. Malipo ya tuzo hii ni malipo makubwa kuwahi kufanywa na RFJ nchini Phillipines tangu mradi huu ulipoanzishwa.

 • Tunaweza kuhakikisha vipi kwamba mmeshalipa tuzo kama hamtoi maelezo dhahiri?

  Tunaweza kuhakikisha vipi kwamba mmeshalipa tuzo kama hamtoi maelezo dhahiri?

  • Kama ilivyoelezewa, RFJ mara kwa mara inatoa matangazo kiasi kuhusu tuzo za malipo ya wahalifu muhimu. Pia tunapeleka ripoti ya siri kwa Bunge baada ya malipo kutolewa.

 • Kitu gani unapaswa kufanya ili upate tuzo? Aina gani ya taarifa unazoziangalia?

  Kitu gani unapaswa kufanya ili upate tuzo? Aina gani ya taarifa unazoziangalia?

  • Mtu yoyote ambaye anatoa habari ambayo itatusaidia ama kuzuia au kuzuia kwa ufanisi vitendo vya ugaidi wa kimataifa dhidi ya Marekani popote hapa duniani huenda akastahili kupewa tuzo.

   Ikiwa, kwa mfano, gaidi anayehusika ama katika kupanga au kutekeleza shambulizi dhidi ya Wamarekani na/ au mali zao atakamatwa au kushtakiwa kutokana na habari iliyotolewa na chanzo, chanzo hicho huenda kikastahili kupewa tuzo.

   Kwa kuongezea, mtu yoyote mwenye habari kuhusiana na kujulikana au sehemu ambako yuko kiongozi wa kundi la ugaidi wa kimataifa huenda akastahili kupewa tuzo. Tuzo pia huenda zikalipwa kwa habari kuhusu mtu binafsi au kundi ambalo linasafirisha madawa ya kulevya kwa ajili ya kufadhili vitendo vya ugaidi wa kimataifa au kuchangisha fedha kugharimia au kuunga mkono kundi la kigaidi.

   Hata hivyo, chini ya sheria ambayo inauhusu mpango huu, wafanyakazi wa serikali ya Marekani, majimbo, wilaya na wafanyakazi wa serikali za kigeni kwa ujumla hawawezi kushiriki katika mpango wa tuzo hii kama watatoa habari ambazo wamezipata katika shughuli zao rasmi za kazi.

 • Je itakuwaje kama mtu atahatarisha maisha yake kwa kutoa taarifa kuhusu gaidi na halafu akagundua kwamba maisha yake yako katika hatari? Je RFJ inaweza kutoa ulinzi?

  Je itakuwaje kama mtu atahatarisha maisha yake kwa kutoa taarifa kuhusu gaidi na halafu akagundua kwamba maisha yake yako katika hatari? Je RFJ inaweza kutoa ulinzi?

  • Kama ilivyojadiliwa hapo juu, usiri ni nguzo kuu ya mpango wa RFJ. RFJ itaficha jina la mtu yoyote ambaye anatoa habari kwa kuitikia mwito wa tuzo na/au ambaye amepewa malipo ya tuzo. Kwa kuongezea, kumhamisha mtu huenda kukafanyika kwa mtu na familia yake, lakini masuala haya yatatakiwa yaamuliwe kulingana na kesi kwa kesi.

 • Je watu hulipwa vipi?

  Je watu hulipwa vipi?

  • Kila tuzo itakayoteuliwa itashughulikiwa katika misingi ya kesi kwa kesi. Utaratibu wa malipo ya tuzo ni kama ufuatavyo:

   Aidha idara ya uchunguzi ya kimarekani, kama vile Wizara ya Ulinzi au FBI, au ubalozi wa Marekani uliopo nje ya nchi, lazima kwanza wateue mtu wa kupewa tuzo hii. Na kamati ya idara itafanya tathmini ya kina kuhusu habari iliyotolewa. Ikiwa kamati ya Idara inayohusika na utoaji wa tuzo itaamini kuwa mtu huyo anastahili kupewa tuzo, itapeleka mapendekezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa ajili ya kuidhinisha tuzo hiyo.

   Mapendekezo ya kamati hata hivyo, si ya mwisho. Waziri wa Mambo ya Nje ana maamuzi ya mwisho kuidhinisha au kutoidhinisha tuzo itakayotolewa, na anaweza kubadili fungu la tuzo, kwa kuzingatia misingi ya sheria.

   Kama kuna suala la kihalifu kwenye serikali kuu ya shirikisho katika jambo hili, Waziri atapeleka mapendekezo kwa Mwanasheria Mkuu kabla ya tuzo kutolewa.

 • Je kiwango cha malipo ya zawadi nono kinaamuliwa vipi?

  Je kiwango cha malipo ya zawadi nono kinaamuliwa vipi?

  • Kiwango cha malipo ya tuzo kitatolewa kulingana na vigezo kadhaa,miongoni mwa sababu hizo ni, ikiwa pamoja na ukubwa wa kitisho ambacho kinatolewa na gaidi, ukubwa wa hatari au madhara kwa Wamarekani au mali, ubora wa habari zilizotolewa, na hatari inayomkabili mtoaji habari na familia yake, pamoja na kiwango cha ushirikiano wa mtu huyo katika uchunguzi au kesi.

 • Unaweza kutoa maelezo kuhusu Mfuko wa Tuzo kwa Haki?

  Unaweza kutoa maelezo kuhusu Mfuko wa Tuzo kwa Haki?

  • Mfuko wa Tuzo kwa haki ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa bila faida kulingana na kipengele 501(c)(3) taasisi ya hisani ambayo ina uhusiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Mradi wa Tuzo kwa Haki upo kwa lengo la kuchangisha na kupata michango binafsi kwa ajili ya matumizi katika kutambua na kuwakamata wanaotaka kutenda ugaidi ndani na nje ya Marekani. Mfuko wa Tuzo kwa Haki ulianzishwa na unasimamiwa na kundi la Wamarekani. Kundi hilo liliifuata Wizara ya Mambo ya Nje muda mfupi baada ya mashambulizi ya Septemba 11 na kuomba kuidhinishwa kuchangisha fedha kupitia michango kutoka kwa umma kwa ujumla ili kuisaidia RFJ. Tulilitathmini pendekezo hili na kuunga mkono juhudi za Mfuko wa Tuzo kwa Haki. Maswali ya ziada lazima yaelekezwe kwenye mfuko huo katika mtandao www.rewardsfund.org.

 • Kwa kutoa zawadi nono, je hushawishi watu kujichukulia sheria mkononi?

  Kwa kutoa zawadi nono, je hushawishi watu kujichukulia sheria mkononi?

  • Hatushawishi watu wajichukulie sheria mikononi na watu wengine kutoka taasisi binafsi waanze kuwatafuta na kuwakamata magaidi; badala yake, RFJ inatoa tuzo kwa habari ambazo zitazisaidia mamlaka za serikali kuwapata na kuwakamata watu kama hao.

 • Kama ninataka kutoa taarifa, nawasiliana na nani?

  Kama ninataka kutoa taarifa, nawasiliana na nani?

  • Watu wenye habari lazima wawasiliane na Ofisi ya Usalama katika eneo katika ubalozi wa Marekani au Ubalozi mdogo, FBI au kutuma habari sehemu hii:

   Anwani ya Posta: RFJ, Washington DC 20522-0303, USA Namba ya Simu: 1-800-US-REWARDS. Barua Pepe: [email protected]

 • Ningependa kuomba ruhusa kutumia picha zifuatazo kutoka kwenye mtandao wenu katika kuwasilisha habari hizi au kuchapisha.

  Ningependa kuomba ruhusa kutumia picha zifuatazo kutoka kwenye mtandao wenu katika kuwasilisha habari hizi au kuchapisha.

  • Isipokuwa kama kuna suala la hati miliki, habari katika mtandao huu ni kwa ajili ya umma kuangalia na zinaweza kunakiliwa, kuchapishwa au vinginevyo kutumiwa bila ya ruhusa ya RFJ. Tunaomba RFJ itajwe kuwa ni chanzo cha habari na kwamba picha yoyote lazima ielezewe ilikopatikana au kutajwa imepigwa na nani au mwandishi au RFJ kama inavyostahili.

   Kama hati miliki imeelezewa kwenye picha, mchoro au kitu chochote, ruhusa ya kunakili vitu hivi lazima itolewe kutoka kwa chanzo cha awali. Kwa kuongezea, lazima ieleweke kuwa kuna kipengele cha kihalifu, 18 U.S.C. 713, ambacho kinazuia matumizi ya nembo ya Marekani chini ya misingi hiyo iliyoelezewa katika kipengele hicho; kwahiyo, tunapendekeza kwamba uwasiliane na afisa mhusika kabla ya kutumia nembo hiyo kwa njia yoyote ile.