Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abdullahi Yare

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Abdullahi Yare ni mkuu wa Habari wa al-Shabaab. Pia anafanya kazi kama msaidizi wa Ahmed Abdi aw-Mohamed (Godane), mwanzilishi na amiri-jeshi wa al-Shabaab.

Jamaat-ud-Dawa ni muanzilishi wa Harakat Shabaab al-Mujahdin (al-Shabaab). Alitangazwa hadharani kama amiri-jeshi wa kikundi mnamo Desemba 2007. Aw-Mohamed ameshika jukumu la ukamanda kwaajili ya shughuli za al-Shabaab kote nchini Somalia. Alidai kuwa kikundi chake kilihusika na mauaji ya Mei 2007 ya jaji Beledweyne, Somalia; na mwezi Machi 2007, alipanga mashambulizi dhidi ya vikosi vya jeshi vya Ethiopia nchini Somalia. Pia amefanya kazi kama msaada kifedha kwa al-Shabaab. Mnamo Novemba 20, 2008, Wizara ya Fedha ya Marekani, ilimtaja aw-Mohamed chini ya Kifungu namba 13224, ambacho hulenga magaidi na wote wanaotoa msaada kwa magaidi au vitendo vya ugaidi. Aw-Mohamed alitajwa pia chini ya Kifungu namba 13536 kwa kuchangia vurugu na kudhoofisha hali ya usalama nchini Somalia.

Al-Shabaab ilikuwa ni kikosi cha Kijeshi cha Mahakama ya Kiislamu ya Somalia ambayo ilijitwalia sehemu kubwa ya Kusini mwa Somalia ndani ya nusu ya pili ya mwaka 2006. Al-Shabaab imeendelea na vurugu zake za uasi Somalia-Kusini na Somalia-Kati. Kikundi kimedai kuhusika na milipuko kadhaa, ikiwa ni pamoja na aina mbalimbali za mauaji ya kujitoa mhanga huko Mogadishu na Somalia Kati na Kaskazini, ikilenga hasahasa maafisa wa Serikali ya Somalia na wanaosemekana kuwa Wafuasi wa Serikali ya Mpito ya Muungano (TFG) ya Somalia. Al-shabaab inawezekana ilihusika na wimbi la mfululizo wa milipuko mitano ya kujitoa mhanga kwenye magari mwezi Oktoba, 2008, ambayo kwa wakati mmoja ilipiga maeneo yaliyolengwa kwenye miji miwili Kaskazini mwa Somalia, na kuua watu wasiopungua 26 na kuwajeruhi wengine 29. Al-Shabaab iilihusika na ulipuaji pacha wa jijini Kampala, Uganda, mnamo Julai 11, 2010, ambao uliua zaidi ya watu 70, akiwemo Mmarekani mmoja. Kikundi kinahusika kwa mauaji ya Wahamasishaji wa amani wa Somalia, Wafanyakazi wa Shirika la Misaada la Kimataifa, viongozi kadhaa wa vikundi visivyo vya kiserikali, na waandishi wa habari. Mnamo Februari 2012, al-Shabaab na al-Qaida walitangaza rasmi kushirikiana kwao (kuungana kwao).

Wizara ya Mambo ya Nchi ya Marekani ilikitaja kikundi cha al-Shabaab kuwa kikosi cha Kigaidi cha Uangamizaji wa Wageni, chini ya Kifungu cha Sheria namba 219 cha Uhamiaji na Utaifa (kama kilivyopitishwa) Februari 26, 2008 na ni Kikosi Maalumu cha Ugaidi wa Dunia chini ya Tamko Rasmi Namba 13224, mnamo Februari 29, 2008.