Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abdullah Ahmed Abdullah

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 10

Abdullah ni kiongozi wa ngazi za juu wa al-Qa’ida na mwanachama wa Baraza la uongozi wa al-Qa’ida, ya “majlis al-shura.” Abdullah ni ofisa mshikafedha mwenye uzoefu, mwezeshaji, na mpangaji wa uendeshaji wa al-Qa’ida.

Abdullah alihukumiwa na kushtakiwa na shirikisho la baraza kuu mnamo Novemba 1998 kwa jukumu lake la mabomu katika Ubalozi wa Marekani ndani ya Dar-es-Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya mnamo Agosti 7, 1998. Mashambulizi yaliua raia 224 na kujeruhi wengine zaidi ya 5,000.

Katika mwaka 1990, Abdullah alitoa mafunzo ya kijeshi kwa wafanyakazi wa al-Qa’ida na wanaume wa makabila wa Somalia ambao walipigana dhidi ya vikosi vya Marekani huko Mogadishu wakati wa operesheni ya kurejesha matumaini. Kutoka mwaka 1996-1998, yeye aliendesha kambi nyingi za mafunzo ya al-Qa’ida ndani ya Afghanistan.

Baada ya mabomu ya ubalozi, Abdullah alihamia Irani chini ya ulinzi wa shirika la Kiislamu la mapinduzi la Irani (IRGC). Mwaka 2003 mamlaka ya Irani ilimuweka yeye na viongozi wengine wa al-Qa’ida chini ya kifungo cha nyumbani. Mnamo Septemba 2015, Abdullah na viongozi wengine wa ngazi za juu wa al-Qa’ida waliachiwa na Irani kutoka kizuizini kwa kubadilishana na Mwanadiplomasia wa Iran aliyetekwa na al-Qa’ida ndani ya Yemen.

Picha zaidi za

Picha ya Abdullah Ahmed Abdullah
English AAA and SaA PDF