Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abdul Zakir

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Abdul Rauf Zakir, pia anafahamika kama Qari Zakir, ni mkuu wa operesheni za kujiua wa Mtandao wa Haqqani na kamanda wa operesheni huko Kabul, Takhar, Kunduz, na Majimbo ya Baghlan, Afghanistan. Zakir ni mhusika wa kutoa mafunzo kwa Mtandao wa Haqqani, ambao unajumuisha mafunzo ya silaha ndogo, silaha nzito, na ujenzi wa vifaa vya kulipuka.

Zakir alimfuata kiongozi wa Mtandao wa Haqqani Sirajuddin Haqqani mnamo 2008, kuomba msaada wa kifedha kwa kubadilishana na upanuzi wa hadhi na operesheni za kundi huko kaskazini mwa Afghanistan, na kuwa mshirika wa kuaminika wa Sirajuddin. Amekuwa akihusika mashambulizi makubwa ya kujitoa muhanga ya Mtandao wa Haqqani ambayo kwa upande mmoja yamepelekea maamuzi ya mwisho kama kuendelea au la na mashambulizi makubwa kama yalivyopangwa na makamanda wa wilaya. Mashambulizi kutumia watu walichaguliwa toka kwenye mpango wa mafunzo ya Zakir yanajumuisha mashambulizi ya 2010 dhidi ya kambi za majeshi ya muungano Salerno na Chapman; Shambulio la Juni 2011 katika Hoteli ya Intercontinental, ambalo liliua raia 11 na polisi wawili wa Afghanistan; na Shambulio la Septemba 2011 dhidi ya Ubalozi wa Marekani, Kabul ambalo liliua Waafghanistan 16, kujumuisha watoto sita.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilimtambulisha Abdul Rauf Zakir Gaidi wa Ulimwenguni kupitia Hati Maalum 13224 mnamo Novemba 5, 2012

Mtandao wa Haqqai ni kikundi cha kijeshi kilichoundwa na Jalaluddin Haqqani, Kamanda wa kivita wa Afghanistan kuanzia miaka ya 1980 ambaye alipigana dhidi ya Umoja wa Sovieti. Mtandao wa Haqqani unashirikiana na Taliban na al-Qaida ambao unalenga kuujenga upya utawala wa Taliban nchini Afghanistan. Mtandao wa Haqqani kimsingi umejikita Kaskazini mwa Waziristan, Pakistan, na unafanya operesheni mpakani mwa mashariki ya Afghanistan na Kabul. Wanamtandao wa Haqqain wanatambulika zaidi kama kundi hatari sana la waasi linalolenga Muungano wa majeshi katika Afghanistan.

Mtandao wa Haqqani umepanga na kufanikisha utekaji nyara kadhaa dhidi ya Marekani na Majeshi ya Muungano nchini Afghanistan, pia serikali ya Afghanistan na walengwa wa kiraia. Miongoni mwa mashambulio ya kutisha ya kikundi yanajumuisha shambulio kwenye Hoteli ya Intercontinental huko Kabul Juni 2011, ambalo liliua raia 11 na Polisi wawili wa Kiafghanistan; Bomu la lori la Septemba 2011 huko katika Jimbo la Wardak, Afghanistan, ambalo lilijeruhi wanajeshi 77 wakimarekani; Shambulio la masaa 19 dhidi ya Ubalozi wa Marekani na Makao makuu ya Jeshi la Kimataifa na Usalama (ISAF) huko Kabul mnamo Septemba 2011; Bomu la kujitoa muhanga la June 2012 dhidi ya Kambi ya jeshi ya Salerno, ambalo liliua wanajeshi wawili wa kimarekani na kujeruhi Zaidi ya 100; na Masaa 12 ya kuzingirwa kwenye Hoteli ya Spozhmai huko Kabul mnamo Juni 2012, ambalo lilipelekea kifo cha walau waafghanistan 18, kumuisha raia 14.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilibainisha Mtandao wa Haqqani kama Kundi la Kigaidi la Nje mnamo Septemba 19, 2012.