Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abdul Rahman Yasin

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Abdul Rahman Yasin alimsaidia mpangaji mkuu wa ugaidi Ramzi Ahmed Yousef kufanya mashambulizi mwezi Februari 1993 kwenye jengo la World Trade Center mjini New York. Yosef na Yasi waliendesha gari lililojaa milipuko kwenye eneo la chini la jengo la World Trade Center, watu sita waliuawa na wengine elfu moja kujeruhiwa. Yasin alikimbia Marekani haraka ili kuepuka kukamatwa.

Baada ya mabomu, maafisa wa polisi walipata ushahidi ambao ulisababisha kushtakiwa na kukamatwa kwa washukiwa kadhaa wa ugaidi waliohusika na ulipuaji huo wa bomu, akiwemo Yasin.

Yasin alizaliwa nchini Marekani, na kuhamia Iraq katika miaka ya 1960, na kurejea Marekani kipindi cha majira ya kipupwe mwaka 1992. Ana hati ya kusafiria ya Marekani.

Mtu aliyetajwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Uharibifu kwa kutumia moto au milipuko; uharibifu kwa njia ya moto au milipuko kwa mali za Marekani; kusafirisha kifaa cha mlipuko barabarani; uharibifu wa magari au huduma za magari; njama za kutenda uovu au kuifanyia ubadhirifu Marekani; kusaidia na kushiriki; adhabu ya kifo au kifungo cha maisha, pale kifo kinapotokea; shambulizi kwa afisa wa serikali kuu akiwa kazini; na kufanya uhalifu wa kutumia nguvu kwa kutumia silaha au chombo cha madhara.

Picha zaidi

Abdul Rahman Yasin