Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abdul Saboor

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Abdul Saboor ni mtaalamu wa milipuko anayejihusisha na Hezb-e Islami Gulbuddin (HIG).

Saboor ni mhusika wa Mei 16, 2013 kifaa cha kwenye gari cha kusababisha mlipuko na shambulio la kujitoa muhanga huko Kabul, Afghanistan, ambao uliangamiza gari la kivita lisiloingiza risasi la Marekani, kuua wanajeshi wawili na wakandarasi wanne wa Kimarekani ambao ni raia, Waafghanistani wanane – kujumuisha watoto wawili – na waliojeruhiwa walau 37.

Saboor na mtaalamu wa milipuko ya HIG Abdullah Nowbahar walikuwa wahusika wakuu katika shambulio SVBIED la Septemba 18, 2012 dhidi ya basi lililowabeba wafanyakazi wa kigeni wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kabul, ambapo zaidi ya dazeni ya watu waliuawa.