Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abderraouf Ben Habib Jdey

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Abderraouf Jdey, ambaye pia anajulikana kama Farouq al-Tunisi, ana historia ndefu ya uhusiano na makundi yenye misimamo mikali. Amekuwa akihusishwa kwa karibu na washirika wa al-Qaida na kuhusika na mipango ya kufanya utekaji nyara/operesheni za kigaidi. Jdey ni mshirika wa mshukiwa gaidi raia wa Tunisia, Faker Boussora, na huenda watu hao wawili walisafiri pamoja katika siku zilizopita.

Jdey aliondoka nchini kwake Tunisia mwaka 1991 na kuhamia Montreal, Canada, na kuwa raia wa Canada mwaka 1995. Wakati akiwa Canada, Jdey alisomea baiolojia kwenye Chuo Kikuu cha Montreal na kuhudhuria Msikiti wa Assuna huko Montreal.

Jdey aliondoka Canada mwaka 1999 na kupatiwa mafunzo ya mapambano na kupata ujuzi nchini Afghanistan mpaka mwaka 2000. Alijihusisha katika mapambano dhidi ya Afghan Northern Alliance na aliandika barua ya kujitoa mhanga ikielezea azma ya kuwa mfia dini katika vita vya jihad. Wakati huo, Jdey pia alionekana katika kanda maarufu ya video ya kujitoa mhanga ambayo baadae iligundulika katika nyumba ya kiongozi wa al-Qaida mwaka 2001.

Baada ya kurejea Montreal mwaka 2001 ambako Jdey alishirikiana na wenye msimamo mkali juu ya njia za kujiunga na jihad, Jdey aliondoka Canada. Mamlaka bado zina wasi wasi kwamba Jdey huenda akajaribu kurejea Canada au Marekani kupanga au kushiriki shambulizi la kigaidi.

Picha zaidi za

Picha ya Abderraouf Ben Habib Jdey
Picha ya Abderraouf Ben Habib Jdey